TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Dar es Salaam, Tanzania — PigaBet leo imetangaza ushirikiano mpya na Fountain Gate FC, hatua inayoendeleza dhamira ya kampuni hiyo katika kukuza mpira wa miguu nchini Tanzania pamoja na kuendeleza michezo kama chachu ya mshikamano wa jamii, shughuli za kiuchumi na hadhi ya taifa.
Ushirikiano huu unaashiria mwanzo wa hatua mpya muhimu kwa Fountain Gate FC wakati klabu hiyo inaanza enzi mpya katika jiji la Arusha, ambalo sasa ni makazi yake mapya. Mbali na kuipa klabu jukwaa imara zaidi la ukuaji, hatua hiyo pia inaiweka Fountain Gate FC ndani ya jiji lenye umuhimu unaozidi kuongezeka katika soka la Tanzania, wakati Arusha ikiendelea kujijenga kama moja ya vituo muhimu vya michezo nchini kuelekea AFCON 2027. Wakati huo huo, Arusha ikiendelea kuimarisha nafasi yake kama kitovu cha michezo na utalii, PigaBet imesema ushirikiano huu unaakisi dhamira ya pamoja ya kuimarisha ushindani wa muda mrefu wa klabu hiyo huku ukichangia pia kasi ya maendeleo ya mpira wa miguu jijini Arusha na Tanzania kwa ujumla.
PigaBet imethibitisha kuwa makubaliano hayo ya udhamini yana thamani ya TZS bilioni 1, jambo linaloonesha ukubwa wa uwekezaji wake katika soka la Tanzania pamoja na imani yake kwa mustakabali wa Fountain Gate FC.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza ushirikiano huo, Arthur Kazola, Meneja wa Masoko wa PigaBet, alisema:
“PigaBet tunaamini kuwa mpira wa miguu una nguvu ya kuunganisha jamii, kuhamasisha vijana, na kuinua hadhi ya miji na maeneo mbalimbali nchini Tanzania. Ushirikiano wetu na Fountain Gate FC unaakisi dhamira yetu ya kuendelea kuunga mkono maendeleo ya mchezo huu na kuzisaidia klabu zenye maono ya wazi ya kukua.”
Aliongeza:
“Fountain Gate FC inaingia katika awamu mpya yenye msisimko mkubwa, huku Arusha ikiwa nyumbani kwao na ikiwa jukwaa imara la kujenga mafanikio zaidi. Tunajivunia kujiunga nao kama mdhamini mkuu wa klabu na kuwa sehemu ya safari hii. Kwetu sisi, huu si udhamini wa kawaida tu — ni uwekezaji katika mustakabali wa mpira wa miguu na katika kukuza hadhi ya Arusha kama jiji la michezo.”
Kazola alisema Tanzania inaendelea kujijengea hadhi kama moja ya mataifa muhimu ya mpira wa miguu barani Afrika, na kwamba mafanikio hayo yanastahili kuungwa mkono kwa uthabiti na sekta binafsi.
“Tanzania inaendelea kukuza hadhi yake kama taifa la mpira wa miguu barani Afrika, na mafanikio hayo yanastahili kuungwa mkono kwa nguvu na kwa mwendelezo. PigaBet tunajivunia kuwa sehemu ya safari hiyo kwa kuwekeza katika klabu, kuunga mkono maendeleo ya mchezo, na kuchangia ukuaji wa mfumo mzima wa soka nchini.”
Rais wa Fountain Gate FC, Japhet Makau, ameukaribisha ushirikiano huo na kusema kuwa athari zake zitakwenda mbali zaidi ya klabu yenyewe.
“Nawashukuru PigaBet kwa uwekezaji huu katika soka la Tanzania. Ushirikiano huu hautaisaidia tu Fountain Gate FC, bali pia utachangia ukuaji wa mpira wa miguu nchini kwa upana wake. Ujio wa PigaBet unathibitisha kuwa soka la Tanzania limekuwa chanzo halisi cha ajira na fursa, hususan kwa vijana wetu. Kwa kushirikiana na PigaBet, tunawakaribisha pia wadau wengine kujitokeza na kuunga mkono maendeleo ya mpira wa Tanzania.”
PigaBet imesema ushirikiano huu utasaidia ukuaji wa Fountain Gate FC ndani na nje ya uwanja, pamoja na kuiwezesha klabu hiyo kuimarisha ushirikiano wake na mashabiki pamoja na wadau mbalimbali.
Ushirikiano huo utaonekana rasmi kwa mara ya kwanza tarehe 9 Aprili 2026, wakati Fountain Gate FC itakapokuwa mwenyeji wa Simba SC katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambao unatarajiwa kuwa tukio muhimu kwa klabu, mashabiki wake na jiji la Arusha kwa ujumla.
Kazola alisema mchezo huo utakuwa fursa muhimu ya kuitambulisha rasmi ushirikiano huo kwa mashabiki na kwa jamii pana ya soka.
“Tunafurahi kuzindua rasmi uwepo wetu na Fountain Gate FC katika mchezo wa nyumbani dhidi ya Simba SC tarehe 9 Aprili katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Huu utakuwa wakati muhimu kwa klabu na ishara thabiti ya imani yetu katika ushirikiano huu na katika uwezo wa Fountain Gate FC kufikia mafanikio makubwa.”
PigaBet imeendelea kujijengea rekodi imara ya kuunga mkono michezo nchini Tanzania, na inaona ushirikiano huu na Fountain Gate FC kuwa sehemu ya dhamira yake pana ya kuchangia kwa maana maendeleo ya mpira wa miguu nchini.
Mwisho
Mawasiliano kwa Vyombo vya Habari
Idara ya Masoko, PigaBet
Dar es Salaam, Tanzania
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment