" POLISI RUVUMA WAWAKAMATA WATUHUMIWA WA MAUAJI YA DEREVA BODABODA

POLISI RUVUMA WAWAKAMATA WATUHUMIWA WA MAUAJI YA DEREVA BODABODA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linawashikilia  watuhumiwa wawili wanaofahamika kwa majina Saidi saidi Ramadhani, Miaka 28 Mkazi wa Mshangano- Namanyigu na Gamaliel Mundo, Miaka 36, Mkazi wa Mtyangimbole kwa tuhuma ya kumuua Lucas Msongela, Miaka 32, Dereva bodaboda, Mkazi wa Mkuzo Songea. Watuhumwa hao walitenda kosa hilo, tarehe  18.03.2026 majira ya usiku  baada ya kumteka mwendesha pikipiki huyo na kumpeleka Peramiho kisha kumshambulia  kwa kutumia  kitu butu na kusababisha kifo chake.Hata hivyo baada ya ufuatiliaji jeshi la polisi limebaini kuwa watuhumiwa hao walikuwa wakijihusisha na matukio mbalimbali ya uhalifu ikiwa ni pamoja na uvunjaji na wizi wa Pikipiki Wilaya ya Songea.Aidha,katika hatua nyingine jeshi la polisi limefanikiwa kumkamata Michael Ngonyani, Miaka 38, Mkazi wa Mtyangimbole ambaye alikuwa akijihusisha na uhalifu wa aina mbalimbali ikiwa pamoja na wizi wa magari Mkoani wa Mbeya na baada ya kupekuliwa mahali alipokuwa akiishi alikutwa akiwa na vitu mbalimbali vidhaniwavyo kuwa vya wizi ambavyo ni;- i. Gari aina ya Toyota  IST  namba T.829 DYH,ii. Leseni 04 za Udereva zenye majina ya watu tofautitofauti, iii. Sound bar 01 aina ya sky wood,iv. Television 02, Inch 65 na 55v. Water pump  01Vilevile mtuhumiwa huyo alikutwa akiwa na Sare za Jeshi la Polisi (kaki) pea moja na Sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Suruali  01 na T-shirt 01, ambazo ailkuwa akizitumia  kufanyia uhalifukatika  maeneo mbalimbali kwa kujifanya askari wa majeshi hayo.  Upelelezi zaidi unaendelea kujua namna mtuhumia alivyopata sare hizo.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

 
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post