
Na Mapuli Kitina Misalaba
Baadhi ya wamiliki wa vyombo vya moto mjini Shinyanga
wamelalamikia ubora wa mafuta waliyonunua katika kituo kimoja cha mafuta,
wakidai kuwa yalichanganywa na maji hali iliyosababisha magari yao kupoteza
nguvu mara baada ya kujaza.
Wakizungumza leo Aprili 7, 2026, baadhi yao wamesema
waligundua hitilafu hizo muda mfupi baada ya kujaza mafuta, huku magari
yakianza kuonyesha dalili zisizo za kawaida kabla hata ya kuondoka kituoni.
Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa, Karimu Ally,
amethibitisha kupokea malalamiko hayo na kusema uchunguzi unaendelea kubaini
ukweli wa tukio hilo.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga,
SACP Janeth Magomi, amesema polisi kwa kushirikiana na EWURA wanafanya
uchunguzi wa kina ili kubaini kama mafuta hayo yalikuwa na dosari.
Wananchi wametakiwa kuwa watulivu wakati uchunguzi ukiendelea, huku mamlaka zikiahidi kutoa majibu rasmi baada ya kukamilika kwa uchunguzi huo.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment