
Watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Dodoma kwa tuhuma za kumuua dereva wa bodaboda, Omary Bakari (21), mkazi wa Michese jijini humo.
Inadaiwa kuwa marehemu alichomwa na kitu chenye ncha kali shingoni na mgongoni kwa lengo la kunyang’anywa pikipiki yake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gallus Hyera, amesema Aprili 1, 2026 wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuwa tukio hilo lilitokea Machi 21, 2026 majira ya saa tatu na nusu usiku katika mtaa wa Chinyoya, kata ya Kilimani.
Amesema baada ya tukio hilo, Jeshi la Polisi lilifanya msako na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja, Sadick Jonathan (23), katika kijiji cha Mazase wilayani Chamwino akiwa na pikipiki ya marehemu yenye namba MC 556 FPE, aina ya Sinoray, rangi nyeusi.
Kwa mujibu wa Hyera, mtuhumiwa huyo alikiri kutenda kosa hilo akishirikiana na wenzake wawili, Paulo Abiel (26) na Ramadhani Hamidu (35), ambao walikamatwa walipokuwa wakijaribu kutoroka kuelekea mikoa jirani.
Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limefanikiwa kudhibiti mtandao wa wizi wa mifugo kwa kuwakamata watuhumiwa 12 katika maeneo tofauti ya jiji hilo.
Miongoni mwa waliokamatwa ni Kedmon Steven na wenzake 11, ambao wanadaiwa kujihusisha na unyang’anyi wa kutumia silaha, kuchinja mifugo waliyoiba na kuisambaza kwenye maeneo ya biashara ili kujipatia kipato kisicho halali.
Aidha, baadhi ya wafanyabiashara wanaodaiwa kushirikiana na mtandao huo kwa kununua na kuuza mifugo au nyama hiyo nao wamekamatwa.
Jeshi la Polisi limesema watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment