" BODABODA SOLWA WAOMBA NIACHEKONA CUP IFANYIKE MARA MBILI KWA MWAKA

BODABODA SOLWA WAOMBA NIACHEKONA CUP IFANYIKE MARA MBILI KWA MWAKA

Maafisa Usafirishaji maarufu bodaboda wa kata ya Solwa, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wamepongeza mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yanayoendelea katika uwanja wa Mwabenda wakisema yamekuwa chachu ya kukuza uchumi pamoja na kuongeza shughuli za usafirishaji katika eneo hilo.

Wakizungumza na Misalaba Media, Maafisa Usafirishaji hao maarufu bodaboda wamesema tangu kuanza kwa mashindano hayo wamekuwa wakipata wateja wengi wanaokwenda na kutoka uwanjani kufuatilia michezo hiyo.

Aidha wamempongeza mwandaaji wa mashindano hayo Paul Daud Augustino (MC NIACHEKONA) kwa kuendelea kuibua vipaji vya vijana pamoja na kuhamasisha umoja na mshikamano kupitia michezo.

Pia wameomba mashindano hayo ikiwezekana yafanyike mara mbili kwa mwaka kutokana na manufaa makubwa yanayoendelea kupatikana kwa wananchi pamoja na vijana wa eneo hilo.

Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yanaendelea kuvuta mashabiki wengi ndani na nje ya Mkoa wa Shinyanga huku yakitajwa kuwa miongoni mwa mashindano yanayochochea maendeleo ya michezo ya vijana katika eneo la Solwa.

Kwa huduma za ushereheshaji wa shughuli mbalimbali, matangazo pamoja na burudani unaweza kuwasiliana na MC NIACHEKONA kupitia namba 0757 267 738.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post