Na, Egidia Vedasto,Misalaba Media, Arusha.Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Joseph Mkude, ametoa wito kwa taasisi na mashirika mbalimbali kuendeleza desturi ya kuunga mkono juhudi za maendeleo katika jamii, hususan katika mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya.Mkude amesema hayo katika hafla ya kukabidhi vitanda kwa nyumba za upataji nafuu (Sober Houses) mkoani Arusha, vilivyotolewa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa ushirikiano na mifuko ya hifadhi ya jamii ya NSSF na PSSF.Amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau imeendelea kuimarisha huduma kwa waraibu na watu wenye matatizo ya akili katika hospitali zote za wilaya nchini, kwa lengo la kuhakikisha taifa linakuwa na watu wenye afya imara na akili timamu.Katika msaada huo, jumla ya vitanda 80 na magodoro 160 vyenye thamani ya Shilingi milioni 43 vimetolewa kwa nyumba mbalimbali za upataji nafuu mkoani humo ili kusaidia huduma za tiba na uangalizi kwa waraibu.Aidha, Mkude amesema nyumba 19 za upataji nafuu mkoani Arusha zimehudumia waraibu 505, ambapo asilimia kubwa ni vijana."Iwapo vijana wengi wataendelea kuathiriwa na uraibu, taifa haliwezi kufikia malengo yake ya ukuaji wa uchumi na maendeleo".Pia amewapongeza waanzilishi na wasimamizi wa nyumba hizo pamoja na familia zinazowapeleka ndugu zao kupata tiba, huku akitoa rai kwa vijana kuepuka matumizi ya dawa za kulevya na kuwataka wafanyabiashara wa dawa hizo kuacha mara moja biashara hiyo kwani mkono wa sheria hautawaacha.Hafla hiyo imebeba kaulinbiu “Kataa dawa za kulevya, timiza malengo yako,”Mmoja wa vijana waliopata nafuu ya matumizi ya dawa za kulevya Michael Adam (38) ameishukuru serikali kuanzisha nyumba hizo ambazo zimesaidia kuokoa maisha ya vijana wengi walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya."Najutia maisha yangu yaliyopita, naumia kwa nini nilijiingiza huko, lakini namshukuru sana Mungu aliyeongoza familia yangu pamoja na wasamalia wema waliohakikisha naondokana na kutumia dawa za kulevya" amesema Michael.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment