Na Osama Mohamedi,Mbinga Madiwani wa Halmashauri ya Mji Mbinga wametakiwa kuwa wabunifu katika kutafuta vyanzo vipya vya mapato ili kusaidia halmashauri kuongeza ukusanyaji wa fedha na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi. Wito huo umetolewa katika baraza la madiwani robo ya tatu kilicholenga kujadili mwenendo wa mapato na maendeleo ya miradi mbalimbali ya wananchi.Akizungumza katibu tawala wa wilaya mbinga Bi.Daniel Pendo amesema kuwa kuelekea tamati ya mwaka wa fedha, madiwani na watendaji wanapaswa kuongeza juhudi katika ukusanyaji wa mapato kwa kuhakikisha wanavuka makadirio waliyojiwekea. Amesisitiza umuhimu wa kuweka mikakati madhubuti itakayowezesha kufikiwa kwa zaidi ya asilimia 100 ya makusanyo ya mapato ya ndani.Amesema shughuli nyingi za maendeleo na uendeshaji wa halmashauri zinahitaji fedha za kutosha, hivyo ni muhimukushirikiana kutafuta vyanzo vikubwa na endelevu vya mapato vitakavyosaidia kuimarisha huduma za kijamii kwa wananchi wa Mbinga Mji.Aidha, madiwani wamehimizwa kuwahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za Mbio za Mwenge wa Uhuru unaotarajiwa kupokelewa 17/ mwezi huu, kwani huleta hamasa ya maendeleo pamoja na kuimarisha mshikamano wa kijamii.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mbinga, Suzo, amewataka wananchi wanaoishi karibu na chanzo cha maji cha MYANGAYANGA kuhakikisha wanakilinda kwa kuepuka shughuli za uharibifu wa mazingira zinazoweza kusababisha chanzo hicho kupotea.lengo ni kulinda chanzo hicho ili kiendelee kuwa suluhisho la kudumu la upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa Mbinga Mji.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254






Post a Comment