" Tanzania Yashuka Nafasi 22 katika Uhuru wa Habari, Bado ya Pili Afrika Masharik

Tanzania Yashuka Nafasi 22 katika Uhuru wa Habari, Bado ya Pili Afrika Masharik

Edwin Soko.Licha ya Tanzania kuporomoka kwa nafasi 22 kwenye kuheshimu uhuru wa Habari imeshika nafasi ya pili kwa Nchi za Afrika ya Mashiriki kwenye kuheshimu uhuru wa habari.Nimeisoma kwa umakini ripoti ya viwango vya kuheshimu uhuru wa habari (Press Freedom Index Ranking 2026) inayotolewa na Shirika la Kimataifa la Reporters Without Boarders(RSF) kupitia tovuti yal https://rsf.org/en/2026-rsf-index-press-freedom-25-year-lowRipoti hiyo inaonyesha Tanzania imeporomoka kwa nafasi 22 kutoka kuwa ya 95 kati ya Nchi 180 (95/180) kwa Mwaka 2025 na kuwa ya 117 kati ya Nchi 160 (117/180).Licha ya kuporoka kwa nafasi hizo 22 bado Tanzania imekuwa  Nchi ya pili nyuma ya Kenya iliyoshika nafasi ya 106  kati ya Nchi 180 kwenye kuheshimu uhuru wa habari  Duniani na kuwa  ya kwanza kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hatua hiyo hiyo ni hatua ya kupongezwa lakini lazima ziwepo jitihada za ziada kwenye kuimarisha uhuru wa habari zaidi.Pia kushuka kwa nafasi hizo 22 kwa Tanzania kumepimwa kwenye viashiria vitano muhimu kwenye zoezi la kupima uhuru wa habari. *kiashiria cha kisiasa* Tanzania imeshuka toka pointi 95 kwa Mwaka 2025 hadi pointi 117 kwa mwaka 2026. *kiashiria cha uchumi,* Tanzania imeshuka toka pointi 87 kwa mwaka 2025 hadi pointi 112 kwa mwaka 2026. *Kiashiria cha kisheria* , Tanzania imeshuka toka pointi  113 kwa mwaka 2025 hadi pointi  ya 120 kwa mwaka 2026. *Kiashiria cha kijamii,* Tanzania imeshuka toka pointi 92 hadi kwa mwaka 2025  pointi 112  kwa mwaka 2026. *Kiashiria cha kiulinzi*  *na usalama* , Tanzania imeshuka toka pointi 107 kwa mwaka 2025  hadi pointi 121 kwa mwaka 2026.Wakati nafanya ichambuzi huu niligusia kidogo nafasi ya yetu Tanzania na Nchi nyingine za Afrika mashariki, kwa uchambuzi wa kitakwimu au namba na pointi, *Kenya* inaongoza kwa kushika nafasi ya kwanza ukanda wa Afrika ya Mashariki kwa kuwa ya kwanza kwa kushika  nafasi ya 106/180 kwa mwaka 2025 toka nafasi ya 117/180 kwa mwaka 2025.(Imepanda) *Tanzania* ya pili kwa kushika nafasi ya 117/180 kwa mwaka  toka nafasi ya 95 kwa mwaka 2025 (imeshuka). *Sudani ya kusini* imeshika  nafasi ya tatu kwa kushika nafasi  ya 118/180 kwa mwaka 2026 toka nafasi ya 109 kwa mwaka 2025 (Imepanda *Burundi* imekuwa ya nne  kwa kwa kushika nafasi  ya 119/180 kwa mwaka 2026 toka nafasi ya 125/180 kwa mwaka 2025 (Imepanda). *Somalia* imeshika nafasi ya tano  kwa kuwa ya 126/180 kwa mwaka 2026 toka nafasi ya 136/180 kwa mwaka 2025 (imepanda). *Uganda*  imeshika nafasi ya saba kwa kuwa ya 131/180 kwa mwaka 2026 toka nafasi ya 143/ 180 kwa mwaka 2025.(imepanda) *Rwanda*  imeshika nafasi ya nane na mwisho katika ukanda wa Afrika ya mashariki kwa kuwa ya 139/180 kwa mwaka 2026 toka nafasi ya 146/180 kwa mwaka 2025 (imepanda).pia kwa kutaka upate uelewa zaidi  nimerahisisha kwa kukuwekea Nchi 10 bora za Afrika zilizofanya vyema kidunia katika kuheshimu uhuru wa habari kama ifuatavyo.South Africa nafasi  21Namibia (23)Cabo Verd(30)Ghana (39)Gabon (41)Seychelles (45)Gambia (46)Mauritania (50)Mauritius (51)Liberia / Sierra Leone (52)Pia Nchi tatu zilizofanya vizuri kwenye kuheshimu uhuru wa habari Kidunia ni Norway, Uholnzi na Estonia.Ripoti hiyo pia imebainisha kuwa Mwaka huu 2026 ndio mwaka mbaya kutokea kwenye historia ya miaka 25 iliyopita, kwa upande wa madhila jumla ya waandishi wa habari 25 wameuawa kuanzia Januari 2026 hadi sasa.Ni matumaini yangu  kuwa, uhuru wa habari unahitaji jitihada za pamoja kati ya serikali, Wanahabari, Taasisi za habari, na wadau wengine wa vyombo vya habari pamoja na jumuiya ya kinataifa.Tuungane kwa pamoja kwenye kuyapinga matukio yanayoathiri Nchi yetu kwenye kuheshimu uhuru wa habari, kama vile kinyimwa kwa taarifa, kamatakamata ya waandishi wahabari, uzimaji wa intaneti, fungia fungia vyombo vya habari, kutungwa kwa sheria kandamizi na matumizi mabaya ya taasisi za usimamizi wa vyombo vya habari, yote hayo yanakwamisha nia njema ya serikali  ya kuwa na Nchi huru yenye kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari.Natumai kuwa, jitihada za mheshimiwa Rais Samia Suluhu  kwenye kujenga vyombo vya habari huru na vyenye nguvu ya kiuchumi kupitia  ripoti ya uchumi ndani  vyombo vya habari itafanyiwa  kazi na kuboresha maslahi ya vyombo vya habari na wanahabari wa Tanzania kwa ujumla.Nia yake njema ya kufungulia vyombo vya habari iendelezwe  kwa dhati katika kuheshimu vyombo vya habari .Maadili na miiko ya uandishi wa habari ni muhimu sana katika sekta yetu.Tukumbuke tuna wajibu wa ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kutafuta taarifa, kuchakata na kutoa taarifa ila tukumbuke na ibara ya 30 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ninayosisigiza " bila kuathitinhaki ya mtu mwingine".Naweka kalamu yangu pembeni nikitoa rai kuwa tushikamane kwenye kulinda uhuru wa vyombo vya habari ili mwakani 2027 tuwe kwenye nafasi ya juu ya kuheshimu uhuru wa habari. *kwa maoni.* Edwin SokoMchambuzi wa HabariMwalimu wa Habari 0754551306Mwanza

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254




 

Post a Comment

Previous Post Next Post