" KASULU TC YAADHIMISHA SIKU YA WAJANE DUNIANI, WAJANE WAHIMIZWA KUVUNJA UKIMYA

KASULU TC YAADHIMISHA SIKU YA WAJANE DUNIANI, WAJANE WAHIMIZWA KUVUNJA UKIMYA

Maadhimisho ya Siku ya Wajane Duniani kwa ngazi ya Mkoa wa Kigoma yamefanyika katika Halmashauri ya Mji Kasulu ambapo wajane wamehimizwa kuwa na ujasiri wa kuwasilisha changamoto zinazowakabili ili zipatiwe ufumbuzi wa haraka.

Akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Fatina H. Laay wa Halmashauri hiyo, Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Kigoma Epheta Msiga amesema maadhimisho hayo yanalenga kutoa fursa ya kuibua, kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili wajane na makundi mengine maalumu katika jamii.

Kwa upande wake, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Mji Kasulu Lucy Njovu amesisitiza umuhimu wa malezi na makuzi bora kwa watoto ili kuwajengea maadili mema, nidhamu na hofu ya Mungu na kuwa raia wema.

Katika hatua nyingine, Afisa Maendeleo ya Jamii na Mratibu wa Mikopo ya Asilimia 10 wa Halmashauri hiyo, Godfrey Jeremiah amehamasisha wananchi kuunda vikundi na kujisajili ili kunufaika na mikopo mbalimbali inayotolewa na Serikali huku akiahidi kutoa ushirikiano na ushauri wa karibu kupitia Maafisa Maendeleo ya Jamii katika kata zote.

Aidha, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Novatus Peter amewahimiza wajane na wanawake wote wanaokabiliwa na changamoto za kisheria kufika katika Dawati la Msaada wa Kisheria ili kupata ushauri, msaada wa kisheria na kuwezeshwa kupata haki zao kwa mujibu wa sheria.

Kila mwaka ifikapo tarehe 23 Juni Dunia huadhimisha Siku ya Wajane Duniani kwa lengo la kuhamasisha jamii kutoa msaada, kutetea haki zao na kukomesha unyanyapaa pamoja na dhuluma wanazokumbana nazo wajane ulimwenguni kote.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post