
Serikali imetangaza hatua kubwa katika kuwawezesha vijana kiuchumi nchini kupitia utengenezaji wa mfumo mpya wa kidijiti ambao umefikia asil...
Serikali imetangaza hatua kubwa katika kuwawezesha vijana kiuchumi nchini kupitia utengenezaji wa mfumo mpya wa kidijiti ambao umefikia asilimia 90 ya utekelezaji wake.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka, alibainisha bungeni kuwa mfumo huo utafanya kazi kama Kituo cha Huduma Jumuishi (One-Stop Center) ili kutambua ujuzi, mahitaji, na maeneo wanakotoka vijana.
Mfumo huu unaunganishwa na taasisi muhimu kama Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), pamoja na taarifa za wahitimu wa vyuo vya VETA ili kuwaunganisha vijana na fursa za ajira na kuwawezesha kimkakati.
Katika kukabili changamoto za ajira, sehemu ya mkopo wa shilingi bilioni 200 iliyoahidiwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeelekezwa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) kwa ajili ya kuendeleza viwanda vidogo na kongani za viwanda katika kila wilaya.
Hatua hii inaenda sambamba na jitihada za kuwaandaa vijana kushindana katika soko la kimataifa kupitia sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Serikali kupitia sera yake ya kidijiti na mashirikiano na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), inahuisha vituo vya vijana kama vile Kituo cha Tehama cha Ilonga mkoani Morogoro, ambacho kinajihusisha na teknolojia za kisasa ikiwemo uchambuzi wa data, akili munde (AI), na robotiki ili kukuza vipaji vya vijana na kusambaza taarifa za fursa hadi vijijini kupitia maofisa maendeleo.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment