Wahitimu wa Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Kasulu wamesisitizwa kutowasahau wazazi na walezi wao waliowawezesha na kuwaunga mkono katika kipindi chote cha masomo yao bali waendelee kuwakumbuka na kuwatunza.Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Mwl. Vumilia Julius Simbeye wakati akifunga rasmi mahafali ya tano ya Chuo cha VETA Kasulu kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Antony Mwakisu yalifanyika katika ukumbi wa chuo hicho.Mwl. Simbeye amesema kuwa njia bora ya kuwashukuru wazazi na walezi ni kutumia maarifa na stadi walizozipata kuboresha maisha yao na familia zao pamoja na kuwatunza walezi wao kwa kadri ya uwezo wao hata kwa kile kidogo watakachokipata.Aidha, Mkurugenzi Simbeye amewashukuru wazazi na walezi kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha kwa Chuo cha VETA Kasulu katika kipindi chote cha masomo ya wanafunzi hao huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiana ili kuchochea maendeleo ya Halmashauri ya Mji Kasulu na Taifa kwa ujumla.Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Ayubu Ngalaba Kilugu ameahidi kuendelea kushirikiana na Chuo hicho katika kuwawezesha wahitimu kunufaika na fursa mbalimbali ikiwemo mikopo ya vikundi ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254




























Post a Comment