Dar es Salaam, Julai 5, 2026 – Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Dkt. Eveline Munisi, ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kuimarisha mahusiano ya kijamii, akisema mahusiano mazuri ni msingi wa kujenga umoja, mshikamano na maendeleo ya taifa.Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), Dkt. Munisi alisema Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano) inaendelea kuwa na mahusiano mazuri na taasisi mbalimbali za kijamii, taasisi za kidini, vyama vya siasa pamoja na asasi za kiraia.Alisema Serikali inatamani kuona jamii ikiendelea kuwa na mahusiano mazuri kwa kuwa ndiyo yanayoweka mazingira rahisi ya kupatikana kwa maendeleo. Alitoa rai kwa wananchi kuendelea kudumisha umoja na mshikamano kama Watanzania.Dkt. Munisi pia alisema Serikali inaendelea kutekeleza maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha Tanzania inaendelea kuzalisha wataalamu wake kupitia wakufunzi wa ndani ili kupunguza utegemezi wa wataalamu kutoka nje ya nchi katika miaka ijayo.Alisema dunia ya sasa inathamini zaidi ujuzi, hivyo Serikali imeendelea na programu mbalimbali za kuwapa vijana mafunzo ya ujuzi. Aliongeza kuwa hivi karibuni alifanya ziara ya kutembelea vyuo mbalimbali kwa ajili ya kukagua maendeleo ya utoaji wa mafunzo hayo.Aidha, alisema ametembelea mabanda ya taasisi mbalimbali zinazoshiriki maonesho hayo, ikiwemo PSSSF, WCF na OSHA, ambapo ameshuhudia namna zinavyotoa elimu na huduma kwa wananchi.Aliwahimiza wananchi ambao bado hawajatembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano) katika Maonesho ya Sabasaba kufika ili kupata huduma na elimu mbalimbali zinazotolewa na ofisi hiyo na taasisi zake.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment