Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limewajulisha wananchi kuwa hali ya mipaka ya nchi na usalama kwa ujumla ni shwari.
Hali hiyo ya utulivu imechangiwa na ari ya kizalendo ya wananchi katika kulinda amani na kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama, jambo linalowawezesha kuendelea na shughuli zao za ujenzi wa taifa bila kikwazo.
Pamoja na kuwepo kwa utulivu huo, jeshi limebaini kuwepo kwa uhamasishaji na upotoshaji unaofanywa na watu wasioitakia mema nchi, wakiwataka wananchi kushiriki vitendo vya vurugu na uvunjifu wa amani.
Watu hao wanajaribu kulichafua jeshi kwa kudai kuwa litahusika kuwalinda wafanya ghasia, jambo linaloweza kusababisha madhara kwa jamii, uharibifu wa mali na kurudisha nyuma uchumi wa taifa.
Kufuatia propaganda hizo, JWTZ linawasihi wananchi kupuuza wito wowote unaohamasisha vurugu na kuwataka kutoshiriki kabisa katika vitendo vya uvunjifu wa amani, bali waendelee na shughuli zao za kila siku bila hofu yeyote.
Jeshi limesisitiza kuwa halitasita kuchukua hatua stahiki kwa yeyote atakayeshiriki vurugu hizo, likikumbusha kuwa Ibara ya 147 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inalipa jukumu la kulinda nchi na wananchi wake.
Aidha, Kifungu cha 22 cha Sheria ya Ulinzi wa Taifa Sura ya 192 linazipa mamlaka kisheria nguvu za kusaidia mamlaka za kiraia pale kunapotokea ghasia na uvunjifu wa amani.
Aidha taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Makao Makuu ya Jeshi, Luteni Kanali Sylvester Mangure huko Dodoma, JWTZ limewaomba wananchi kutoa taarifa za uchochezi au viashiria vya vurugu kwa viongozi wa vijiji, mitaa na vyombo vya ulinzi.
Jeshi limewahakikishia wananchi kuwa litaendelea kutekeleza majukumu yake ya ulinzi wa nchi, katiba na mamlaka ya nchi kwa weledi na utii wa hali ya juu.
Vilevile, limesisitiza kujitolea kwake kuendelea kushirikiana na raia pamoja na vyombo vingine vya usalama ili kudumisha amani, utulivu na umoja kwa ustawi wa taifa.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment