Tonny Alphonce - Misalaba Media .MorogoroWaandishi wa habari na watangazaji wametakiwa kujali tahadhari za kiusalama wakati wakitekeleza majukumu yao,kwani hakuna habari yenye thamani zaidi ya maisha yao.Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha wafanyakazi katika vyombo vya habari Tanzania(JOWUTA), Mussa Juma ameeleza hayo wakati akitoa mada juu ya Ulinzi na Usalama kwa wanahabari Julai 4,2026,katika mafunzo kwa wanahabari wanaotakiwa kwenda kuwafundisha waandishi wengine(ToT) yanayofanyika mjini Morogoro.Mafunzo hayo yameandaliwa na Umoja wa klabu za waandishi wa habari (UTPC) kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la kusaidia tasnia ya habari( IMS) na JamiiAfrica kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya , Ikiwa ni sehemu ya mradi wa Kuwapa Nguvu Waandishi wa Habari kwa ajili ya Jamii zenye Taarifa.Juma amesema ni muhimu wanahabari wanapotimiza kazi zao kuzingatia tahadhali za kiusalama ili wasidhulike ikiwepo kutokuwa na upande katika migogoro,kufanya tathimini za kiusalama kabla kufanya kazi na kuwa na kutofanyakazi kwa kujitenga."Unapokwenda kuandika habari za migogoro,mikutano ya kisiasa, maandamano na mengine jiandae, usiende peke yako,kuwa na mawasiliano ya mhariri wako ama mwanahabari mwingine na wadau wengine wa masuala ya haki za binaadamu ili likitokea tatizo upate msaada wa haraka "amesemaJuma ambaye pia ni Makamu mwenyekiti Arusha Press Club(APC) amesema, waandishi wengi ambao wamekumbwa na madhila ya kiusalama walikuwa peke yao, ama walikuwa wanapendelea upande mmoja wa mgogoro,machawa, ama hawakujali tahadhari za kiusalama.Awali .Mkurugenzi wa Mtendaji wa UTPC, Kenneth Simbaga aliwataka wanahabari wanaopata mafunzo hayo kuyathamini kwani wanatakiwa kwenda kuwafundisha waandishi wengine."Nyie mmepata bahati kubwa kupata haya mafunzo lakini mjuwe yana uwajibikaji nendeni mkafundishe wengine na masuala yote ya usalama wao binafsi na katika matumizi ya mtandao na masuala hali ya maisha yao na kukabiliama msongo wa mawazo"amesemaWaandishi zaidi ya 30 Tanzania bara na visiwani kutoka katika klabu za waandishi mikoani wanatajiwa kupata mafunzo hayo na baadae kuwafundisha wengine.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment