Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limewakamata na linaendelea kuwashikilia watuhumiwa wanne kwa tuhuma za kukutwa wakipanga na kuhamasisha watu kufanya vurugu na uhalifu mwingine katika maeneo mbalimbali ya Jijini Mbeya.

Wanaoshikiliwa ni pamoja na Noah Mwalwange, Mwenyekiti CHASO Mkoa wa Mbeya, Gwamaka Mboka ambaye ni Katibu CHASO Mkoa wa Mbeya, Agustino Wasinyo, Mwenyekiti Tawi la CUoM na Rojas Mpwani, Mwanachuo CUoM.

Watuhumiwa hawa walikamatwa Julai 04, 2026 saa 10 jioni katika eneo la Mafiati lililopo Kata ya Maanga, Jijini Mbeya. Ushahidi unakamilishwa ili hatua nyingine za kisheria zifuatwe dhidi yao.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kutoa wito kwa baadhi ya wananchi kuacha kujiingiza katika vitendo vya kupanga na kuhamasisha uhalifu katika Jiji la Mbeya kwani hatua kali kwa mujibu wa sheria zitachukuliwa dhidi yao.

Imetolewa na:
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254