✅ Wajadili Fursa za Ajira kwa Madereva wa Kitanzania
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Usafirishaji ya MOWASALAT, Ahmad Hassan Al Obaidly, alipofanya ziara katika kampuni hiyo tarehe 8 Julai, 2026, jijini Doha, nchini Qatar.
Aidha, mazungumzo yao yalilenga majadiliano kuhusu kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kampuni ya MOWASALAT katika sekta ya usafirishaji na masuala ya ajira, hususan kuongeza fursa za ajira kwa Madereva wa Kitanzania nchini Qatar.
Katika ziara hiyo, Waziri Sangu aliambatana na Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Mhe. Habibu Awesi Mohamed, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano, Zuhura Yunus, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana, Ajira na Uwezeshaji Zanzibar, Khalid Masoud Waziri, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Uwekezaji, Rashid Ali Salim, pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Ajira, Jane Sorogo.
Post a Comment