
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura amewataka askari polisi kuhakikisha huduma wanazotoa kwa wananchi zinazingatia utu, haki, weledi na huruma, hususan wanaposhughulikia waathirika wa ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto.
Akizungumza jijini Dodoma wakati akifunga Mkutano wa Watendaji wa Madawati ya Jinsia na Watoto kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, sambamba na uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano cha Gender-Based Violence and Violence Against Children na Kitabu cha Mwanafunzi na Mwongozo wa Mwalimu wa Somo la Polisi Jamii, IGP Wambura alisema mafanikio ya jeshi hilo hayapaswi kupimwa kwa idadi ya mikutano au mifumo inayozinduliwa, bali kwa idadi ya waathirika wanaopata msaada na kiwango cha imani ambacho wananchi wanacho kwa jeshi hilo.
Alisisitiza kuwa mafunzo na teknolojia lazima yatafsiriwe katika ubora wa huduma inayozingatia haki na weledi, huku akibainisha kuwa watendaji wa madawati hayo hukutana na watu waliopitia maumivu na hofu hivyo wanapaswa kutekeleza sheria kwa busara na huruma kwani kulinda wanawake na watoto ni msingi wa amani na maendeleo ya taifa.
Aidha, alieleza kuwa vitabu vilivyozinduliwa vitasaidia kuimarisha mafunzo na weledi wa askari, wakati Kituo cha Mawasiliano kitawawezesha wananchi kutoa taarifa kwa haraka, kupata ushauri na kuelekezwa kwenye huduma stahiki, hatua itakayoongeza ufanisi kwa manusura wa ukatili na kuimarisha uhusiano mzuri kati ya Jeshi la Polisi na jamii.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment