" KAMANDA MAGOMI ASISITIZA USHIRIKIANO KATI YA JAMII NA JESHI LA POLISI

KAMANDA MAGOMI ASISITIZA USHIRIKIANO KATI YA JAMII NA JESHI LA POLISI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Janeth Magomi, amekutana na kufanya mazungumzo na wananchi pamoja na vikundi vya Sungusungu katika Kata ya Samuye, Halmashauri ya Shinyanga, kwa lengo la kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na wananchi katika kudhibiti uhalifu.Akizungumza na wananchi hao, SACP Magomi amesisitiza umuhimu wa jamii kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu na matukio ya uhalifu yanayotokea katika maeneo yao.Amesema ushirikiano wa karibu kati ya Polisi na wananchi ni muhimu katika kuhakikisha maeneo yao yanakuwa salama, huku akiwataka wananchi kutokuwa na hofu katika kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa wakati.Aidha, SACP Magomi amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawalinda watoto dhidi ya vitendo vya ukatili na unyanyasaji, akisisitiza kuwa jamii haipaswi kuvumilia aina yoyote ya unyanyasaji dhidi ya watoto au watu wa rika lolote.Pamoja na hayo, SACP Magomi amesisitiza umuhimu wa wananchi na vikundi vya Sungusungu kuzingatia sheria katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu, hususan wakati wa kuwakamata watu wanaotuhumiwa kujihusisha na uhalifu. Amewataka kuepuka kujichukulia sheria mkononi na badala yake kuwafikisha watuhumiwa katika vyombo vya dola kwa ajili ya hatua za kisheria.
Vilevile, amewataka wananchi kuhakikisha wanajilinda na kujihakikishia usalama wao kwanza wakati wanapokabiliana na matukio ya uhalifu, badala ya kujiweka katika hatari ya kujeruhiwa au kupoteza maisha. Amesisitiza kuwa jukumu la wananchi ni kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi na kushirikiana na vyombo vya usalama kwa njia salama na inayozingatia sheria.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post