
Jumuiya ya Kifalme ya Afrika (League of United Kingdom of Africa - LUKA) imepongeza uamuzi wa Serikali ya Tanzania wa kuwashirikisha wataalamu wa sheria na majaji kutoka nchi nyingine za Afrika katika Tume ya Uchunguzi wa Kijinai inayochunguza matukio ya vurugu na uhalifu yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Katika tamko lake, Jumuiya hiyo imesema kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kuimarisha uwazi, weledi, uadilifu na imani ya wananchi katika mchakato mzima wa uchunguzi, huku ikieleza kuwa taasisi za kitaifa zinapokabiliana na masuala yenye uzito mkubwa kwa taifa, zinaweza kunufaika pakubwa kupitia uzoefu na utaalamu wa wataalamu kutoka mamlaka nyingine barani Afrika.
Kufuatia hatua hiyo, LUKA imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Serikali yake kwa kufungua milango na kuruhusu wataalamu kutoka nchi za nje ya Tanzania kushiriki bega kwa bega katika mchakato huo wa kitaifa.
Aidha, Jumuiya imefafanua kuwa ushiriki wa majaji na wataalamu hao kutoka nje ya nchi haupaswi kutafsiriwa kwa namna yoyote ile kama ishara ya kutokuamini mfumo wa sheria na haki wa Tanzania, bali imeitazama hatua hiyo kama dhihirisho la kujiamini, ukomavu wa taasisi za nchi, na utayari wa kutumia mitazamo jumuishi ya kisheria katika kushughulikia masuala yenye maslahi mapana kitaifa na kimataifa.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment