Mkoa wa Kigoma umeibuka mshindi katika maonesho ya wakulima 88 Kanda ya Magharibi kwa mwaka 2026 kwa kushika nafasi ya kwanza na ya pili, maonesho yaliyofanyika katika Viwanja vya Ipuli, Manispaa ya Tabora.Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza imetangazwa kuwa mshindi wa 1 kwa kundi la Mamlaka za Serikali za Mitaa ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe imeshika nafasi ya pili wakati Halmashauri ya Wilaya ya Igunga iliyopo Mkoa wa Tabora imeshika nafasi ya 3.Mgeni rasmi na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Afya) Mhe.Dr Jafar Rajab Seif amekabidhi vyeti kwa washindi, zawadi na Kikombe cha ushindi kwa mshindi wa kwanza na mshindi wa pili na kusisitiza kuwa maonesho ya wakulima ni darasa muhimu linalowapa fursa wakulima, wafugaji na wajasiriamali kutumia teknolojia hivyo waendelee kuzalisha bidhaa zenye ubora na viwango ili kukidhi soko la ndani na nje ya nchi.Naibu Waziri Dkt. Jafar amesisitiza eneo la Maonesho ya 88 Kanda ya Magharibi kuwa kituo cha ubora (center of excellence) na kuwaagiza Tanroads na Tarura kuweka miundombinu imara katika eneo hilo la maonesho Ipuli ili litumike mwaka mzima siyo wakati wa maonesho tu.Aidha, maonesho hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Kaimu mkuu wa Mkoa wa Tabora na Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Balozi Simon Sirro, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi , Makatibu Tawala,Wakuu wa Idara na Taasisi za Serikali,Wadau na Wananchi kutoka maeneo mbalimbali.Maonesho hayo yamefungwa rasmi leo Jumamosi Agosti 8, 2026 na Mhe.Dr Jafar Rajab Seif, Naibu Waziri - TAMISEMI (Afya) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maonesho hayo ya wakulima kanda ya magharibi kwa mwaka 2026.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254













Post a Comment