Katika ulimwengu wa sasa ambapo idadi ya vijana imekuwa kubwa kutokana na kuboreka kwa huduma za afya na uwepo wa amani, suala la ajira limekuwa changamoto kuu inayohitaji ushirikiano wa dhati kutoka kwa wadau wote badala ya kutumiwa kama chambo cha kisiasa.
Hivi karibuni, Dkt. Ayoub Rioba Chacha alizungumzia hili kupitia mtandaoni akisisitiza jinsi juhudi za baadhi ya wanasiasa zinavyoelekea kuhamasisha uhadhina miongoni mwa vijana, jambo ambalo ni hatari kwa usalama, utulivu, na maelewano ya nchi yetu.
Alisema Vyama vya upinzani na vya ushindani vinapaswa kutambua kuwa havipo kwa ajili ya kuwa upinzani daima, bali vinatekeleza jukumu la kutafuta dola, na hivyo vinapaswa kuenenda kwa staha na uzalendo wakifahamu kuwa hii ni nchi na inapaswa kulindwa.
Hatari kubwa inayojitokeza ni pale vyama vinapo chochea vijana na kuwajengea chuki dhidi ya waliopo madarakani kwa kuwafundisha kuwa wanaweza kuwaondoa kwa njia yoyote ile, jambo ambalo huzaa mazingira ya hovyo ambayo yanaweza kurudi kuwatafuna viongozi hao hao pindi watakapofanikiwa kushika dola.
Kama msemo unavyosema kwamba mchimba kisima huangukia mwenyewe, chama kinachowapandikiza vijana roho ya fujo na kutokuwa na staha kinaweka mtego wake mwenyewe, kwani vijana hao hao waliotengenezwa kuwa wakali na wasioridhika hawatasita kugeukia utawala mpya iwapo ahadi za uongo hazitatimizwa ndani ya muda mfupi.
Ni muhimu basi kwa vyama vyote vya siasa kuachana na tabia hii ya kupanda mbegu za chuki na badala yake kujikita katika kujenga siasa za hoja, staha, na suluhu za kudumu za changamoto za kiuchumi ili kulinda usalama na kusonga mbele kama taifa moja lenye mshikamano.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment