Maafisa usafirishaji maarufu kama bodaboda katika Manispaa ya Shinyanga wamepewa elimu kuhusiana na tabia ya kutorosha pikipiki iliyopata ajali kutoka eneo la tukio pindi ajali inapotokeaElimu hiyo imetolewa na Mkaguzi wa Polisi Emmanuel Mwaitenga akiambatana na Sajenti Ibrahimu Lukumbo katika kituo Cha Maafisa usafirishaji eneo la Kiwanda Cha Jambo ambapo amewataka Maafisa usafirishaji hao kushirikiana na Jeshi la Polisi pindi ajali inapotokea na kutunza vyombo vya moto vilivyohusika kwenye ajali ili taratibu za kisheria ziweze kufuatwa na waliohusika kwenye ajali waweze kupata haki zao.Mkaguzi wa Polisi Mwaitenga amewaeleza kuwa vitendo vya kuficha vyombo vya moto kutoka kwenye ajali ilipotokea ni kosa kisheria lakini pia inaweza kumnyima haki yake mtu aliyesababishiwa ajali.Kupitia elimu hiyo Kwa upande wao Maafisa usafirishaji hao wameahidi kushirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha wanatoa ushahidi wa matukio ya ajali yanayotokea pamoja na kulinda vyombo vya moto vinavyohusika na ajali za barabarani.PROFESSOR MGOKO EPISODE 2
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment