Meneja Mkazi wa Barrick nchini , Dkt. Melkiory Ngido akisalimiana na wananchi na wazee wa kimila wa Kijiji cha Kiseriani kata ya Engikaret , Wilaya ya Longido mara baada ya uzinduzi wa ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi ya Shikinzi wilayani Longido.
Meneja Mkazi wa Barrick nchini, Dkt. Melkiory Ngido akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kiseriani Kata ya Engikaret Wilaya ya Longido katika uzinduzi wa ujenzi wa madarasa na nyumba za walimu mradi uliofanikishwa na Kampuni ya Barrick nchini.
Meneja Mkazi wa Barrick nchini, Dkt. Melkiory Ngido na Mbunge wa Jimbo hilo na Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa.
Sehemu ya madarasa
Kampuni ya Barrick inayoendesha shughuli zake kwa ubia na serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga Minerals imeunga mkono nguvu ya wananchi wa kijiji cha Kiseriani Kata ya Engikaret Wilaya ya Longido Mkoani Arusha na viongozi wao kufanikisha ujenzi wa madarasa na miundombinu ya shule ya msingi Shikinzi kukabiliana na changamoto ya wanafunzi wa eneo hilo kutembea umbali mrefu kutafuta elimu na pia kuhatarisha maisha yao kutokana na kupita kwenye maeneo yenye wanyama wakali wa porini.
Akizungumza katika uzinduzi wa Shule hiyo Kijiji hapo Meneja Mkazi wa Barrick nchini, Dkt. Melkiory Ngido amesema kutokana na mkakati wa kampuni kuhakikisha inawekeza katika sekta ya elimu, imeguswa na changamoto ya watoto wa eneo hilo kutembea kilomita 32 kwenda na kurudi shule kila siku na imeamua kuunga mkono jitihada za kukabiliana na changamoto hiyo.
“Tunajivunia kama Barrick kuwa kwenye safari hii ya maendeleo ya elimu hapa nchini na ni ahadi tutaendelea kushirikiana na Serikali katika kufanikisha watoto wa Kitanzania wanapata elimu katika mazingira bora na rafiki zaidi,” amesema Dkt. Ngido.
Amesema Barrick itaendelea kushirikiana na wananchi katika kujenga miundombinu ya elimu kwa kuwa wananchi wameonyesha nia ya dhati ya ushirikiano na uadilifu mkubwa katika ujenzi wa madarasa mawili na ofisi ya mwalimu ambapo kampuni imechangia zaidi ya shilingi milioni 180 ambazo zimetumika vizuri kufanikisha lengo lililokusudiwa la kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora katika mazingira rafiki.
Dkt. Ngido ametoa pongezi kwa wananchi wa Kijiji cha Kiseriani ambao wengi wao ni wa jamii ya kifugaji ya Kimasai na viongozi wao kwa kujitoa kuhakikisha mradi huu wa ujenzi wa shule unafanikiwa na kuwaasa kuendelea kuwapeleka watoto wao shule kwa kuwa elimu ndiyo njia ya kuvunja mzunguko wa umaskini na kuwawezesha watoto kujitegemea.
Kwa upande wake , Mbunge wa Jimbo hilo na Naibu Waziri wa Madini, Dkt Steven Kiruswa aliishukuru Barrick ambayo kwa kuwa mwekezaji anayeweka mbele kufanikisha miradi yenye kuleta manufaa katika jamii nchini kote hususani katika sekta za elimu, afya, maji na ujenzi wa miundombinu ya barabara.
Amesema ataendelea kushirikiana na wananchi wa jimbo hilo kutekeleza miradi mbalimbali ya kuboresha maisha ya wananchi ambapo ametoa ahadi ya kutoa mifuko 100 ya saruji katika ujenzi wa madarasa mengine mapya katika shule hiyo na amewashukuru wananchi kwa kujitoa kwa mchango wa nguvu kazi kwa kusomba mawe mchanga na kokoto.
Barrick pia inaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kuboresha sekta ya elimu kupitia fedha za uwajibikaji kwa jamii (CSR) katika maeneo yanayozunguka migodi yake ya North Mara na Bulyanhulu.
Vile vile kwa kushirikiana na Serikali inatekeleleza mradi Barrick-Twiga Future Forward Education Program kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 70 kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa madarasa, mabweni na matundu ya vyoo katika shule za sekondari nchini kote.
Mradi huu ambao umeingia katika awamu ya pili unalenga kujenga madarasa 1,090, majengo ya maliwato na vyoo 1,640 na mabweni 270 katika shule 161 nchini kote ili kuwezesha watoto wa kitanzania kupata elimu katika mazingira bora zaidi ya kujifunza na kufundishia kwa pande zote, walimu na wanafunzi.
Tangu mwaka 2020, baada ya Twiga Minerals kuundwa, Barrick imekuwa ikishirikiana na Serikali katika kuendeleza sekta ya madini ili iweze kuleta tija na maendeleo endelevu kwa taifa.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254








Post a Comment