" CHIFU ANTONIA SANGALALI AWATAKA WANANCHI KUJIANDAA KUKABILIANA NA MVUA ZA EL NIÑO

CHIFU ANTONIA SANGALALI AWATAKA WANANCHI KUJIANDAA KUKABILIANA NA MVUA ZA EL NIÑO

Mwenyekiti wa Machifu Tanzania na Mtemi wa Himaya ya Jigoku, Chifu Antonia Sangalali, amewataka wananchi kuchukua tahadhari na kujiandaa mapema kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua zinazohusishwa na hali ya El Niño.

Chifu Sangalali ametoa wito huo wakati wa Tamasha la 19 la Himaya ya Jigoku, Masela, Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, akiwataka wananchi kutunza chakula na kuchukua tahadhari dhidi ya uwezekano wa kutokea kwa mafuriko katika maeneo mbalimbali.

Amesema wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi wanapaswa kuwa makini na kuondoka mapema endapo wataona hali ya mvua kubwa inayoweza kuhatarisha usalama wao.

“Kuna mvua za El Niño zinazoelezwa kutokea mwaka huu. Tutakuwa na mafuriko, niwaombe tunzeni chakula, mjiangalie sana, chukueni tahadhari mapema. Mkiona mvua za El Niño, mtoke sehemu hatarishi,” amesema Chifu Sangalali.

Taarifa ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) iliyotolewa Agosti 18, 2026, inaeleza kuwa msimu wa mvua za Vuli wa Oktoba hadi Desemba 2026 unatarajiwa kuathiriwa kwa kiwango kikubwa na hali ya El Niño yenye nguvu kubwa.

Chifu Sangalali amesisitiza kuwa maandalizi ya mapema ni muhimu ili kulinda maisha ya wananchi, chakula na mali zao dhidi ya athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua hizo.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post