Juliana BuzurugaChama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini kimemtangaza Juliana Buzuruga kuwa Katibu wa CCM Kata ya Ndembezi, baada ya kushinda uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi hiyo iliyokuwa wazi.Akitangaza Matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi huo Bi Doris Kibabi amemtangaza Buzuruga kushinda kwa kupata kura 22, dhidi ya wagombea wengine ambao ni Pastory Manyinyi aliyepata kura 14, Charles Ngeke na Juma Maridadi ambao walipata kura sifuri kila mmoja.Msimamizi wa uchaguzi huo, Doris Kibabi, ambaye pia ni Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Shinyanga Mjini, amesema uchaguzi huo umefanyika kwa mujibu wa taratibu za CCM, kwa lengo la kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Pendo Sawa, baada ya kuchaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Ndembezi.Jumla ya wapiga kura 36 walishiriki uchaguzi huo na kwamba kura zote 36 zilipigwa, na hakuna kura iliyoharibika.Uchaguzi huo umefanyika leo Septemba 21,2026 katika Ofisi ya CCM Kata ya Ndembezi

PROFESSOR MGOKO EPISODE 2
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment