Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba amewataka viongozi nchini kuweka pembeni tofauti zao na kujielekeza kikamilifu katika kutatua kero za wananchi badala ya kujihusisha na migongano na minyukano isiyo na tija kwa ustawi wa jamii.
Akizungumza wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani Bahi mkoani Dodoma kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi, Dk. Nchemba alisisitiza kuwa viongozi wanapaswa kutambua wajibu wao kwa wananchi badala ya kujivunia vyeo, huku akionya vikali tabia ya baadhi ya vituo vya afya kuwalazimisha wananchi kuchangisha fedha za mafuta ya magari ya kubebea wagonjwa wakati magari ya serikali yana mafuta.
Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu alitoa maagizo mazito kwa uongozi wa wilaya hiyo kuhakikisha wagonjwa waliopewa rufaa hawasumbuliwi kwa kuchangishwa mafuta ya magari ya wagonjwa.
Dk. Nchemba alitoa zawadi ya kumpandisha cheo aliyekuwa Ofisa Elimu wa Wilaya ya Bahi, Boniface Wilson, na kumteua kuwa Ofisa Elimu wa Mkoa kutokana na jitihada zake kubwa zilizoiwezesha wilaya hiyo kushika nafasi ya kwanza katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba kwa mwaka 2025.
Alisisitiza kuwa serikali inatambua na kuwapa heshima watumishi wote wanaofanya vizuri ili iwe chachu ya uwajibikaji, huku akiwataka viongozi kubadili mienendo yao na kujikita katika kusimamia maendeleo ya wananchi kwa maslahi mapana ya taifa.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment