Na Lydia Lugakila, Mbeya.
Katika kuongeza kasi ya utayari dhidi ya mvua za El Niño, Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Mbeya umepokea zana na vifaa mbalimbali kutoka Wizara ya Ujenzi ili kulinda na kuimarisha mtandao wa barabara mkoani humo.
Akiongea wakati wa kipokea vifaa hivyo mnamo Septemba 18, 2026, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Seleman Bishanga, alipongeza jitihada hizo za Serikali na kubainisha kuwa msaada huo umekuja wakati muafaka.
Alieleza kuwa tayari kikosi kazi chake kimeshaingia mtaani kuanza ukarabati katika maeneo yanayotajwa kuwa hatarishi kwa ajali, ikiwemo Mlima Iwambi na eneo la Simike.
Mhandisi Bishanga alifafanua kuwa lengo kuu la hatua hizo ni kuhakikisha usalama wa wasafiri na kuzuia kukatika kwa mawasiliano ya miundombinu pindi mvua kubwa zitakaponyesha.
“Vifaa hivi tulivyopokea vitatusaidia kutatua dharura mbalimbali zitakazojitokeza wakati wa mvua na tayari tumeanza kufanyia kazi maeneo korofi ili kuweka mazingira salama kwa vyombo vya usafiri,” alibainisha Mhandisi Bishanga.
Wakati huo huo, Bishanga alitoa wito kwa wananchi wote waliovamia na kuweka makazi ndani ya hifadhi ya barabara kuondoka mara moja ili kupisha ujenzi na upanuzi wa miundombinu hiyo.
Hata hivyo alitoa tahadhari kwa wakazi wa maeneo ya mabondeni kuwa waangalifu kutokana na hatari ya mafuriko yanayoweza kusababishwa na mvua hizo.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 2
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652

Post a Comment