.
Na, Egidia Vedasto, Misalaba Media, Arusha.
Msuluhishi wa Malalamiko ya Kodi nchini, Erastus Mtui, amesema wadau walioshiriki mkutano wa TOST wamekubaliana kuanzisha na kuimarisha ushirikiano wa karibu utakaowawezesha kuendelea kubadilishana uzoefu, kujengeana uwezo na kuongeza ujuzi katika utatuzi wa malalamiko ya kodi.
Akizungumza Jijini Arusha wakati akifunga mkutano, Mtui amesema ushirikiano huo pia utasaidia wadau kupitia na kuangalia upya sheria na taratibu zinazowaongoza katika utekelezaji wa majukumu yao, ili kuhakikisha zinakwenda sambamba na mahitaji ya wafanyabiashara, wawekezaji na mazingira ya sasa ya biashara.
Amesema Tanzania imekuwa mfano mzuri wa kuigwa katika suala la ushirikiano baina ya taasisi zinazohusika na masuala ya kodi, akitolea mfano Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambayo imeendelea kushirikiana na wadau katika kuboresha huduma na mifumo ya ukusanyaji wa kodi.
Kwa upande wake.
Mtui amesema "wafanyabiashara wamekuwa wakisifu mifumo ya ukusanyaji kodi inayotumiwa na TRA, na uzoefu huo unaweza kutumika kama msingi wa taasisi nyingine kuimarisha mifumo yao na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi na wafanyabiashara".
Kwa upande wake Mkuu wa Kitivo cha Biashara na Uchumi kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM),Dr. Shaban Ngole, amepongeza kufanyika kwa jukwaa hilo akisema ni hatua muhimu katika kuleta mabadiliko makubwa katika sheria na taratibu zinazohusu utatuzi wa malalamiko ya kodi nchini.
Amesema jukwaa hilo linatoa fursa kwa wadau mbalimbali kukutana, kujadili changamoto zinazowakabili wafanyabiashara na wawekezaji katika masuala ya kodi, pamoja na kutoa mapendekezo yatakayosaidia kuboresha mfumo wa usuluhishi wa malalamiko ya kodi.
"Ushirikishwaji wa taasisi za elimu, wafanyabiashara, Serikali na wadau wengine ni muhimu katika kuhakikisha maboresho yanayofanyika katika sheria na taratibu za kodi yanaendana na mahitaji ya mazingira ya biashara na kuchangia kujenga mfumo wa haki, uwazi na ufanisi katika utatuzi wa malalamiko" Amesema.
Vilevile Katibu Kiongozi mstaafu, Philemon Luhanjo, amesema ni muhimu kuimarisha mahusiano kati ya walipa kodi na taasisi zinazokusanya kodi, akieleza kuwa uhusiano mzuri ni msingi wa kujenga uaminifu na ushirikiano katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Luhanjo amesisitiza kuwa bila kuwa na mahusiano mazuri kati ya mlipa kodi na mkusanya kodi, Serikali inaweza kukosa mapato yanayostahili kutokana na baadhi ya walipa kodi kukosa uelewa, ushirikiano au imani katika mifumo ya ukusanyaji kodi.
Luhanjo amesema "Serikali na taasisi zinazohusika na ukusanyaji wa kodi zinapaswa kuendelea kuweka mazingira rafiki kwa walipa kodi, kusikiliza changamoto zao na kuhakikisha taratibu za kodi zinaeleweka na kutekelezwa kwa haki, jambo litakalosaidia kuongeza utii wa kodi na mapato ya Serikali"
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment