Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeweka lengo la kimkakati la kuzalisha Watanzania wenye ujuzi wapatao milioni 5.8 ifikapo mwaka 2050, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi na kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Anthony Kasore alisema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na wanahabari kuhusu mikakati ya mamlaka hiyo katika kujenga taifa lenye ujuzi, akisisitiza kuwa kuongezeka kwa mahitaji ya nguvu kazi yenye ujuzi katika sekta mbalimbali kumeisukuma mamlaka hiyo kuboresha ubora wa mafunzo na kubuni mbinu mpya ili kuhakikisha wahitimu wanakidhi mahitaji halisi ya soko la ajira la ndani na nje ya nchi.
Kasore alifafanua kuwa VETA itaweka mkazo mkubwa katika kufanya mifumo ya mafunzo kuwa nyumbufu na jumuishi, kuongeza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), kuunganisha mafunzo na uzalishaji, na kuimarisha ushirikiano thabiti na waajiri, viwanda, sekta binafsi, vyama vya kitaaluma na mafundi mahiri ili kujenga uchumi imara, jumuishi na shindani utakaofikia lengo maalum la kuzalisha wahitimu 5,635,529 ifikapo mwaka 2050.
Katika kufanikisha azma hiyo, serikali iko katika hatua za mwisho za kukamilisha ujenzi wa vyuo vipya 65 vya VETA, vikiwamo 64 vya wilaya na kimoja cha Mkoa wa Songwe, ambavyo vinatarajiwa kuanza kutoa mafunzo rasmi Januari 2027 na kuongeza idadi ya vyuo nchini kutoka 80 vya sasa hadi kufikia 145, huku kukiwa na matarajio ya kudahili wanafunzi wapya 130,892 kwa mpigo.
Vyuo hivyo vipya vimepangwa kuwa vituo mahiri vya ukuzaji ujuzi, ajira, kujiajiri, ubunifu na uzalishaji, ambapo vitajikita moja kwa moja katika kutoa mafunzo yanayolenga sekta za kipaumbele ikiwamo kilimo, ujenzi, madini, nishati, TEHAMA, usafirishaji, viwanda na uchumi wa buluu.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment