Wananchi wa Kata ya Somanga wilayani Kilwa wameungana na Serikali kushiriki zoezi la usafi wa mazingira, ikiwa ni hatua ya kujiandaa kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua za El Nino zinazotarajiwa kunyesha.
Zoezi hilo limehusisha usafishaji wa maeneo ya makazi, mifereji ya maji na mazingira yanayozunguka jamii, kwa lengo la kupunguza hatari ya maji kuziba njia, kusababisha mafuriko na kuharibu miundombinu wakati wa mvua.
Viongozi wa Kata ya Somanga wamewahimiza wananchi kuendelea kushiriki katika usafi wa mazingira pamoja na kufuata tahadhari zinazotolewa na Serikali, hususan katika maeneo hatarishi kwa mafuriko.
Aidha, wananchi wametakiwa kuhakikisha mifereji ya maji inakuwa safi, kuondoa taka zinazoweza kuziba njia za maji na kutoa taarifa kwa viongozi pale wanapoona viashiria vya hatari ili hatua zichukuliwe mapema.
Hatua hiyo inaelezwa kuwa sehemu ya juhudi za pamoja kati ya Serikali na wananchi katika kuimarisha usalama wa jamii, kulinda mazingira na kupunguza madhara yanayoweza kusababishwa na mvua kubwa.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 2
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652
Post a Comment