Kampeni ya Ongea na Kamanda imeendelea leo ambapo Kata ya Maganzo imefikiwa kwa mara nyingine.Akiongea na wananchi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Janeth Magomi aliwapongeza wananchi kwa umoja wao uliowafanya kujaa katika mkutano huo.Kamanda Magomi aliendelea kusisitiza suala la ulizi wa amani ili kuendelea kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na kujiepusha na vikundi vinavyohatarisha amani na utulivu.Suala la malezi halikuachwa nyuma, ambapo Magomi aliwataka wananchi kulea watoto katika maadili bora kwa kuzingatia utamaduni wetu. Aliongezea umuhimu wa kupeleka watoto katika nyumba za ibada ili kuwa na kizazi chenye hofu ya MunguKamanda Magomi alikagua ujenzi wa jengo la Sungusungu na kuahidi matifalu elfu moja kuunga mkono ujenzi huo na kukubali ombi la kuwa msimamizi wa jengo hilo kama lilivyoletwa na viongozi wa Sungusungu wa kata hiyo.Aidha Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kishapu, Mrakibu wa Polisi Ester Gesogwe alitumia mkutano huo kutimiza ahadi ya mifuko 16 ya Saruji aliyoahidi. Alisema kuwa huo sio mwisho wa michango yao na kuwa wataendelea kutoa mpaka jengo litakapokamilika.Wananchi nao walitoa shukrani zao kwa Jeshi la Polisi kwa michango yao itakayowezesha ujenzi huo na kuahidi kushirikiana vyema na Jeshi la Polisi


PROFESSOR MGOKO EPISODE 07
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254





Post a Comment