Wahitimu wa mafunzo ya awali ya Jeshi la Akiba (Mgambo) wametakiwa kuwa chachu ya kudumisha amani, usalama na mshikamano katika jamii kwa kuzingatia misingi ya nidhamu, uadilifu na weledi huku wakitekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria na misingi ya haki.Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Mhe. Mtella Allam Mwampamba, aliyekuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya kuhitimisha mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Luteni Kanali Joseph Athanas Murimi.Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Mtella amewataka wahitimu kutumia ipasavyo maarifa na ujuzi walioupata kupitia mafunzo ya kinadharia na vitendo, huku akiwasisitiza kuwa mfano wa nidhamu, uzalendo, uaminifu na uadilifu katika kutekeleza majukumu yao.Mafunzo hayo yamejumuisha mada mbalimbali zikiwemo usalama wa raia, uhamiaji, rushwa, usajili na utambuzi, utimamu wa mwili pamoja na masuala ya zimamoto.Akisoma risala kwa niaba ya wahitimu, Albert Kayanda amesema mafunzo hayo yamewaongezea maarifa na ujuzi muhimu utakaowawezesha kulitumikia taifa kwa kuisaidia jamii katika masuala mbalimbali ya kiusalama.Aidha, amewahakikishia viongozi na wananchi kuwa wahitimu watatekeleza majukumu yao kwa uaminifu na uadilifu, sambamba na kushiriki kikamilifu katika kulinda na kudumisha utulivu wa jamii.Kwa ujumla, wahitimu 65 wa Jeshi la Akiba wamehitimu mafunzo hayo yaliyoanza tarehe 01 Julai 2026 na kuhitimishwa rasmi tarehe 30 Oktoba 2026 ktika uwanja wa mpira uliopo Kata ya Murufiti, Halmshauri ya Mji Kasulu.

PROFESSOR MGOKO EPISODE 07
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



















Post a Comment