Mwananchi akihakiki na kuthibitisha taarifa za mali zake katika zoezi la disclosure linalofanyika katika eneo la Mgeo, Kigoma, linalohusisha maeneo yaliyoathiriwa na Mradi wa SGR Lot 6. Zoezi hilo linampa mwananchi fursa ya kujiridhisha na taarifa za mali zake, kutoa hoja au marekebisho pale inapobidi, na kuthibitisha taarifa hizo kabla ya hatua zinazofuata za mchakato wa uthamini na ulipaji wa fidia.
KIGOMA
Wananchi 344 kati ya 346 waliofika katika zoezi la disclosure katika Mtaa wa Mgeo, Kata ya Buhanda, Kigoma, wameridhia fidia zao na kusaini fomu za kuthibitisha uhakiki wa taarifa zao za mali zinazohusika na mradi wa SGR.
Mthamini Mwandamizi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rashid Mageta, amesema wananchi hao ni sehemu ya jumla ya wananchi 370 waliofanyiwa uthamini katika eneo hilo.
Amesema hadi sasa wananchi 346 wamefika kuhakiki taarifa zao, ambapo 344 wameridhia fidia na kusaini fomu za uhakiki, huku wananchi wawili wakieleza kutoridhishwa na fidia walizoainishiwa.
“Wananchi 344 wameridhia fidia na kusaini fomu za uhakiki wa taarifa zao. Wawili hawajaridhia fidia, huku wananchi 24 kati ya 370 waliofanyiwa uthamini bado hawajafika kuhakiki taarifa zao,” amesema Mageta.
Amesema zoezi hilo bado linaendelea ili kuwapa fursa wananchi 24 ambao hawajafika kushiriki katika uhakiki wa taarifa zao na kutoa hoja pale wanapoona kuna taarifa zinazohitaji marekebisho au ufafanuzi.
Mageta amesisitiza kuwa ushiriki katika zoezi la disclosure ni hatua muhimu katika mchakato wa uthamini, kwa kuwa humpa mwananchi fursa ya kuona na kuhakiki taarifa za mali yake pamoja na taarifa zinazohusiana na fidia.
Ameongeza kuwa wananchi wanaohusika wanapaswa kutumia fursa hiyo kuhakiki taarifa zao na kutoa hoja kwa wakati, hatua inayosaidia kubaini na kushughulikia changamoto mapema kabla ya kukamilika kwa mchakato wa uthamini na ulipaji wa fidia.
Aidha, amewahimiza wananchi 24 ambao bado hawajafika kushiriki katika zoezi hilo ili kuhakiki taarifa zao na kuhakikisha taarifa zao zinakuwa sahihi kabla ya hatua zinazofuata za mchakato wa mradi wa SGR.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 04
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
















Post a Comment