Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Mwl. Vumilia Julius Simbeye, amefungua rasmi mafunzo ya siku mbili kwa viongozi wa dini na wazee maarufu wa jamii yenye lengo la kuongeza uelewa na kuimarisha juhudi za kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii.Mafunzo hayo yatafanyika kuanzia tarehe 07 hadi 08 Novemba 2026 katika ukumbi mdogo wa mikutano wa Halmashauri hiyo , yakiratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA).Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo, Mwl. Simbeye amewataka washiriki kuyatumia maarifa watakayoyapata kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii kwa kukemea vitendo vya ukatili, kupaza sauti dhidi ya wahusika na kuendelea kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kujiepusha na aina zote za ukatili.Aidha, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano katika masuala ya malezi na makuzi ya watoto ili kujenga jamii yenye misingi bora ya maadili, uwajibikaji na inayolinda haki na usalama wa watoto.Kwa upande wake, mwezeshaji wa mafunzo hayo ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Bi. Amina Kaniki, amewataka viongozi wa dini kutumia majukwaa yao ya kiimani kuelimisha waumini, kuhimiza hofu ya Mungu na kuwajenga katika misingi ya maadili mema pamoja na kujiepusha na vitendo vya ukatili.Katika hatua nyingine, washiriki wa mafunzo hayo wameishukuru Serikali na UNFPA kwa kuandaa mafunzo huku wakiahidi kutumia nafasi zao katika jamii kuwa mabalozi wa kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kuachana na vitendo vinavyochochea ukatili wa kijinsia.Mafunzo hayo yamejikita katika mada kuu ya kutokomeza ukatili wa kijinsia katika jamii, ambapo washiriki wanapata elimu kuhusu maana, aina na madhara ya ukatili wa kijinsia, nafasi na wajibu wa jamii katika kuzuia na kupambana na vitendo hivyo.

PROFESSOR MGOKO EPISODE 07
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254















Post a Comment