" MSIGWA AIPANDISHA SANGU KIMAFANIKIO, KALOWA AWEKA NGUVU KWENYE MAABARA

MSIGWA AIPANDISHA SANGU KIMAFANIKIO, KALOWA AWEKA NGUVU KWENYE MAABARA



Na Lydia Lugakila - Misalaba Media,MBEYA

Mafanikio ya kitaaluma na nidhamu yanayoendelea kuimarika katika Shule ya Sekondari Sangu jijini Mbeya yameendelea kuipa shule hiyo nafasi ya kutambulika, huku juhudi za uongozi wake chini ya Mkuu wa Shule, Jacob Msigwa, zikivutia wadau wa elimu kujitokeza kuunga mkono maendeleo yake.


Katika kuunga mkono juhudi hizo, Afisa Madini wa Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Oscar Kalowa, ameahidi kutoa Sh milioni 4 kwa ajili ya ujenzi wa maabara, hatua inayolenga kuimarisha mazingira ya kujifunzia na kufundishia hususan katika masomo ya sayansi.

Ahadi hiyo inaongeza nguvu katika safari ya maendeleo ya shule hiyo, ambayo imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kuboresha miundombinu na mazingira ya elimu ili kuwawezesha wanafunzi kupata maarifa katika mazingira yanayokidhi mahitaji yao.

Akizungumza katika mahafali ya 62 ya Kidato cha Nne yaliyofanyika Novemba 5, 2026, katika Ukumbi wa Tughimbe jijini Mbeya, Kalowa aliipongeza shule hiyo kwa mafanikio inayoyapata na kuonesha utayari wake wa kuchangia ujenzi wa maabara kupitia ahadi ya fedha hizo.


Kwa upande wake, uongozi wa shule chini ya Jacob Msigwa umeendelea kusimamia juhudi za kuimarisha taaluma, nidhamu na maendeleo ya miundombinu, ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu katika mazingira bora.

Mafanikio mengine yanayoendelea kuonekana katika shule hiyo ni ujenzi wa jengo la utawala, ukarabati wa baadhi ya majengo pamoja na ongezeko la wanafunzi wanaojiunga na Kidato cha Kwanza.

Mahafali hayo yalihusisha jumla ya wanafunzi 120 waliohitimu Kidato cha Nne, ikiwa ni sehemu ya safari yao ya elimu kuelekea hatua nyingine za maisha.

PROFESSOR MGOKO EP 07

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254






Post a Comment

Previous Post Next Post