" SENETI MKOA WA SHINYANGA WAHAMASISHA VIJANA KULINDA AMANI NA MAADILI YA KITANZANIA

SENETI MKOA WA SHINYANGA WAHAMASISHA VIJANA KULINDA AMANI NA MAADILI YA KITANZANIA

Na Edington Mukiza Ezron, Misalaba Media

Vijana wa vyuo wameaswa kuwa na nidhamu na kuepuka vitendo visivyofaa ikiwemo mapenzi ya jinsia Moja(ushoga)ili kuendelea kulinda taifa dhidi ya mmomonyoko wa maadili.

Hayo yamesemwa na  Mwenyekiti wa Seneti Mkoa wa Shinyanga Jackson Aloyce Mwizarubi katika hotuba yake aliyotoa Leo katika chuo Cha serikali za mitaa Shinyanga ambapo umefanyika uchaguzi wa viongozi wa tawi katika chuo hicho.

Mwizarubi ameeleza kuwa vijana wa CCM wanapaswa kuwa na nidhamu na kulinda maadili ya Tanzania kwani wao ndiyo viongozi wa baadae watakaoendeleza ilani ya chama hicho ambapo ameeleza kuwa bila nidhamu hawawezi kupata viongozi bora.

Pia amesema kuwa vijana wanatakiwa kuacha kujihusisha na vitendo vya uchochezi ili kuendelea kulinda amani ya taifa.

Naye Katibu wa Seneti Mkoa wa Shinyanga Lukomanga Jinyage amesema kuwa vijana hao wanatakiwa kuwa karibu na chama hicho ili kuweza kuweka urahisi kwao hasa kupata ajira Kwa urahisi pindi wanapomaliza masomo yao.

Hata hivyo wametakiwa kuwa viongozi bora katika jamii wanayoishi na kuwa na uhusiano mzuri na viongozi mbalimbali ili kujifunza na kupata uzoefu wa kutongoza Kwa misingi iliyo Bora.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post