Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, anatarajiwa
kuwasili Mkoani Shinyanga kesho Jumapili, Novemba 8, 2026, kwa ziara ya kikazi itakayohusisha
Halmashauri zote sita za mkoa huo.
Ziara hiyo inalenga
kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, kusikiliza kero za
wananchi pamoja na kuzungumza na viongozi na wananchi kuhusu masuala mbalimbali
yanayohusu maendeleo ya mkoa huo.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita,
amesema maandalizi ya kumpokea Waziri Mkuu yamekamilika na kuwataka wananchi
kujitokeza kwa wingi kumpokea.
Kwa mujibu
wa ratiba iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Waziri Mkuu ataanza ziara yake
katika Wilaya ya Kishapu kesho, Novemba 8, kabla ya kuendelea na maeneo mengine
ya mkoa huo.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 07
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment