Na Moshi Ndugulile, Shinyanga
Jaji kiongozi wa Tanzania na kamishna
wa tume ya utumishi wa Mahakama Nchini
Mheshimiwa MUSTAPHER SIYANI amewataka
wadau wa Mahakama wakiwemo watendaji hasa
mawakili kujiandaa katika matumizi ya mfumo wa tehama kama daraja la
utoaji haki Nchini
Akitoa mada kuhusu ushiriki wa wadau
katika jukumu la utoaji wa haki kwenye Mkutano kati ya tume ya utumishi wa
Mahakama pamoja na wadau wa Mahakama wa Mkoa wa Shinyanga,ikiwa ni sehemu ya
ziara ya tume ya utumishi wa Mahakama katika Mikoa ya Shinyanga na Simiyu, alisema
dhamira ya Mahakama ya Tanzania ni
kuhakikisha kwamba inapunguza na hatimaye kuachana na matumizi ya analojia
katika shughuli zake,kuongeza uwazi na uwajibikaji kwa kuongeza kasi ya utoaji
haki kwa kuimarisha matumizi ya tehama
‘’ umuhimu
wa wadau wa Mahakama kujiandaa katika matumizi kamili ya Tehama kama daraja la
utoaji haki Nchini,wadau wa Mahakama hasa wale wanaoshiriki uendeshaji wa
Mashauri Mahakamani ,kama ofisi ya Taifa ya Mashitaka,ofisi ya wakili Mkuu wa
serikali,chama cha mawakili Tanganyika na wananchi wote wenye mashauri
Mahakamani,ni vema wakakumbuka kila mara kwamba Mahakama imedhamiria kupunguza
na hatimaye kupunguza matumizi ya karasi,kuongeza uwazi na uwajibikaji kwa
kuongeza kasi ya utoaji haki kwa kuimarisha matumizi ya tehama,jambo hili
limekuwa likisemwa kuhusu dhamira ya mahakama katika matumizi kamili ya
teknolojia hiyo ifikapo Mwaka 2025,manake katika hatua zote kuanzia
usajili,usikilizwaji na utoaji wa hukumu Mahakama itumie teknolojia,amesema jaji
kiongozi Siyani
Mahakama imechukua
hatua kadha wa kadha ikiwemo usimikaji wa mifumo mbalimbali ya kielektroniki,lakini imeunganisha Mahakama
kwenye mkongo ya Taifa,vitendea kazi mbalimbali vimenunuliwa ,kwa ujumla
miundombinu mbalimbali imewekwa hata katika magereza zetu sehemu mbalimbali za
Nchi yetu, wote tujiandae mawakili wote
wa kujitegemea na wale wa serikali wajue kwamba wakati umefika sasa wa kutumia
teknolojia na kuachana na mazoea yale ya kwamba shahidi ni lazima afike
Mahakamani ,umwandae na kasha umwongoze
akiwa mbele yako kumbe unaweza kufanya hivyo kwa kutumia teknolojia,kwa hiyo
matarajio yetu ni kwamba wadau wetu wote wanaohusika na uendeshaji wa mashauri
mahakamani hawatabaki nyuma na kwamba wataweka mipango na kuchukua hatua
sawasawa na mahakama kuelekea matumizi ya tehama.’’ameeleza
Aliwataka mahakimu na mawakili kuwa na juhudi za pamoja kuharakisha mchakato wa utoaji haki kama takwa la kikatiba ili kupunguza au kuondokana kabisa na mlundikano wa mashauri ikiwemo 3419 yaliyopo katika ngazi mbali mbali za mahakama hapa Nchini.
‘’ni jukumu la wadau wetu kuhakikisha
Mahakama inaondokana na Mlundikano wa mashauri , tunaposema mlundikano wa
mashauri tunamaanisha nini ? kwa
Mahakama kuu shauri lolote ambalo limekaa zaidi ya miezi 24 ( kwa maana ya
Miaka miwili )hili ni shauri linaitwa mlundikano kwa kuwa limekaa kwa muda
mrefu ,kwa Mahakama za hakimu Mkazi na Wilaya shauri ambalo limekaa zaidi ya
miezi 12 ( Mwaka mmoja ) hilo ni shauri
la mlundikano,na kwa Mahakama za Mwanzo shauri ambalo limekaa kwa miezi
sita,kwa hiyo ni wazi kwamba bado tunayo mashauri ya mlundikano Mahakamani, ameeleza
Hadi kufikia leo Novemba 21,2022
Mahakama kuu ya Tanzania ina ina jumla ya mashauri 1107 ya mlundikano,Mahakama
za hakimu mkazi jumla ya mashauri 1129,na Mahakama za mwanzo mashauri 10, huku Mahakama za watoto kuna jumla ya
mashauri ya mlundikano 12,kwa hiyo kuna takribani jumla ya mashauri 3419 ya
mlundikano kwenye mahakama za ngazi mbalimbali kuanzia Mahaka kuu ya Tanzania
mpaka za chini .
‘’pamoja
na jitihada mbalimbali zinazoendelea
kufanyika ili kuharakisha mchakato wa utoaji haki kama takwa la kikatiba,ni
muhimu mawakili wasomi wasitumie mbinu za kiufundi kuchelewesha haki , wakati
majaji na mahakimu wakichukua hatua mahsusi kuyasikiliza na kumaliza mashauri
ya muda mrefu wadau na wadaawa wasiwe kikwazo,na badala yake waisaidie Mahakama
kutimiza jukumu lake ,lakini namna nyingine bora ni mawakili kuwasaidia wadaawa
kwa kuwawekea mazingira ya kupatana,wananchi watambue usuluhishi ni njia
nzuri,na watumie fursa hiyo,matarajio ya Mahakama ni kuwa Mawakili wote na
wasomi wa sheria nchini,watasaidia wananchi hususani wale wenye mashauri
kuelewa umuhimu wa kuhakikisha haki inapatikana kwa wakati,kujenga desturi ya
kutumia usuluhishi,na kutokuwa kikwazo kwa juhudi za Mahakama kumaliza msongamano wa mashauri’’
amesema jaji kiongozi
Ameeleza madhumuni ya ziara hiyo
kwamba pamoja na mambo mengine imelenga kukutana na wenyeviti na wajumbe wa
kamati za maadili za Mikoa na Wilaya ,pamoja na watumishi wa mahakama, lakini
pia ni fursa nzuri ya kuitangaza tume hiyo kwa wadau.
Profesa Ibrahimu Juma alisema katika ziara hiyo jumla ya Mahakama 18,za
ngazi ya Wilaya zitazinduliwa katika maeneo mbalimbali Nchini Ikiwemo katika
Wilaya za Busega na Itilima katika kanda ya Shinyanga ili kuongeza huduma za
utoaji haki kwa wananchi
‘’Vile vile
katika ziara hii tutapata nafasi ya kuzindua Mahakama za Wilaya mpya zipatazo
18,hii itafanyika Novemba 25, hii ni hatua kubwa kwa sabababu kuna maeneo
mengi yalikuwa na changamoto kubwa ya
uhaba wa majengo,ulikuwa ukihitajika ukarabati mkubwa,kwa hiyo kwa muda wa
miaka mitano tumekuwa tukishughulikia ujenzi ,kuhakikisha kila Wilaya Nchini
Tanzania( wilaya 139) zinapata Mahakama
za kisasa kwa ngazi ya Wilaya ,ambapo katika kanda ya Shinyanga tutazindua katika
Wilaya za Busega na Itilima wilayani Simiyu (Mkoa wa Simiyu unahudumiwa na Mahakama kuu ya Tanzania kanda
ya Shinyanga)’’alisema profesa Ibrahimu Juma
Awali
jaji mfawidhi wa Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga Athuman Matuma amesema Mahakama hiyo imekuwa na tija
na ufanisi kutokana na ushirikiano mzuri kutoka kwa wadau mbalimbali
‘’katika Mkoa wa Shinyanga imekuwa
ikipata ushirikiano mkubwa sana katika utendaji wa majukumu yake na shughuli za
kila siku kutoka kwa wadau ,ambao ni muhimu zaidi katika kuisaidia Mahakama kutekeleza majukumu yake ya utoaji
wa haki na hivyo kuimarisha utendaji haki nchini,Mahakama ya Tanzania iliweka
mpango ya kuratibu utekelezaji wa ushiriki wa wadau katika mpango mkakati wake
uliopita wa 2015/2016 mpaka 2019/2020,ambapo ilifanikiwa kupata ushirikiano wa
kutosha ,na hivyo kutekeleza majukumu yake ya utoaji haki ipasavyo.
Vilevile katika mpango mkakati wa
sasa wa 2020/2021 mpaka 2022/2025
tumeweka mikakati ,vipaumbele na malengo mbalimbali ili kuimarisha ushirikiano
na wadau.
Ameshukuru
na kupongeza ofisi ya taifa ya Mashtaka NBS na chama cha wanasheria wa
kujitegemea Tanganyika Law Society kwa ushirikiano wao katika ufunguaji wa
mashauri kwa njia ya mtandao,licha ya kuwepo changamoto kadhaa za
kimtandao,ambapo kwa sasa katika Mkoa wa Shinyanga mashauri yote ya jinai
kutoka ofisi ya taifa ya mashtaka na mashauri yote ya madai kutoka kwa
wanasheria wa kujitegemea yanafunguliwa kwa njia ya mtandao.
Ameshukuru
pia ofisi ya upelelezi ya makosa ya jinai
Mkoa wa Shinyanga kwa kukamilisha
upelelezi kwa wakati ikiwa ni pamoja na mashauri ya mauaji ,kwa sasa takribani
mashauri 130 yamekamilika upelelezi wake ambapo yanasubiri kusikilizwa katika
vikao vya Mahakama kuu.
Ameishukuru
pia ofisi ya taifa ya mashtaka kwa kushirikiana vizuri na ofisi ya upelelezi wa
makosa ya jinai katika kukamilisha
upelelezi wa makosa ya jinai ikiwemo mashauri ya mauaji,ambapo ameishukuru pia
ofisi ya taifa ya mashtaka kwa kutoa ridhaa kwa wakati kwa mashauri ambayo
usikilizaji wake unahitaji ridhaa za Mkurugenzi wa mashtaka,hali kadharika
ameishukuru ofisi ya mashitaka Shinyanga kwa ushirikiano wao katika kufanya
jukumu lao la msingi la uendeshaji wa mashtaka kwa kuzingatia ratiba za
mashauri,kuhudhuria na kushiriki kikamilifu katika vikao vya awali kabla ya
usikilizaji wa mashauri (pre- sessions) na vikao vya usikilizaji wa mashauri (sessions)
kwani bila waendesha mashtaka mashauri mengi ya jinai hayawezi kusonga
mbele,kwa hiyo wamesaidia kwa kiwango kikubwa Mahakama kufikia katika malengo
iliyojiwekea ya kusimamia utendaji wa haki.
Amewashukuru
wazee wa Mahakama pamoja na viongozi wote wa dini ambao wana mchango na jukumu kubwa la kujenga maadili katika jamii ili iweze
kuepuka kutenda makosa ya jinai
na hata kujiepusha na migogoro inayozua
mashauri ya madai,kufanya usuluhishi wa mogoro ya ndoa kabla ya kufikishwa
mahakamani kama inavyoelekeza sheria,na kwamba wameendelea kutoa ushirikiano wa
kutosha kwa Mahakama hivyo kusaidia kuirahisishia wa
kutekeleza majukumu yake.
Kwa
upande wake jaji wa mahakama ya rufani na kamishna wa tume ya utumishi wa
mahakama Dkt. Geraid Ndika amewataka wajumbe wa kamati za maadili za Mkoa na Wilaya kutunza siri za vikao vya
kamati pamoja na taarifa za kamati.
Mheshimiwa
jaji Dkt. Ndika amezitaja baadhi ya changamoto zinazojitokeza wakati wa
utekelezaji wa majukumu ya kamati za maadili za Mkoa na wilaya kuwa ni pamoja
na uelewa mdogo wa wananchi juu ya aina ya malalamiko yanayopaswa kuwasilishwa
kwenye kamati na uwepo wa kamati ili waweze kuzitumia, na kwamba changamoto
nyingine ni kamati kutokutana kama ilivyoelekezwa na sharia kwa kigezo cha
ufinyu wa bajeti lakini pia mabadiliko ya mara kwa mara ya wenyeviti wa kamati na
baadhi ya kamati kutowasilisha kwa tume ripoti za vikao vyao.
Amesema ni muhimu zaidi wajumbe wa kamati kuzingatia muongozo wa uendeshaji wa kamati za maadili hatua ambayo itadumisha nidhamu na kuimarisha utendaji wa haki Nchini.
Post a Comment