Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasili Mjini Bukoba mkoani Kagera, kuangalia zoezi la uokoaji kufuatiia ajali ya ndege ya Shirika la ndege la Precision Air PW-494 iliyotokea mapema hii leo.
Akizungumza na wakazi wa Bukoba
Waziri mkuu ameeleza kuwa shuguli ya uokozi imekamilika na watu 19 wamethibitika kufariki dunia mpaka sasa.
ajali hiyo imetokea wakati ndege hiyo ikiwa katika safari zake za kawaida kutoka Dar es Salaam kuelekea Bukoba wakati watu 26 wakiwa wamenusurika.
Mkuu wa mkoa wa Kagera mh.Albert Chalamila amesema watu wawili kati ya hao 45 hawakuwa wasafiri wa ndege hiyo licha ya kuwa wameokolewa.
"Ndugu zangu katika ajali hii iliyotokea ya kuzama kwa ndege yetu ambayo sasa imeokolewa,tumejitahidi angalau kuivuta kusogea karibu na nchi kavu,sor far ndege hii ilikuwa na abiria 43 kama nilivyosema tangu awali, waziri mkuu wetu yupo katika mkoani Kagera ili kuungana na wananchi wa mkoa huu kuhakikisha watu wote hawa ambao wamepoteza maisha basi wanapata heshima kubwa ya kuagwa chini ya ugeni rasmi wa mweshimiwa waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa tanzania ambaye pia amemuwakilisha mweshimiwa Rais" ameeleza mkuu wa mkoa Ndg,Chalamila.
Mmoja wa wahanga wa ajali hiyo bwana Richard Komba ameeleza kuwa hali ya hewa ilionekana kutokuwa nzuri kwenye mwendo wa kutoka mwanza kwenda Bukoba kitendo kilichopelekea rubani wandege hiyo kutoa taarifa kwa abiria wa ndege hiyo kuwa haitoweza kutua.
"Wakati tunakaribia kushuka ikaonekana hatuwezi kushuka kwaio rubani akalazimika kuzunguka tumeenda mpaka huko maeneo ya Missenyi akatupa taarifa kwamba hali ha hewa sio nzuri mvua inanyesha na kuna mawingu na tulikuwa tunaona"
Kwaio akasema anajaribu kurudi kama bado hali ya hewa itakuwa hivyo itabidi arudishe ndege Mwanza, tukawa tunarudi kwa ajili ya kutua tukatangaziwa kabisa kuwa baada ya muda mfupi tutatua lakini bado ya hali ya hewa haikuwa nzuri mtikisiko ulikuwa mkubwa badae tukajikuta tupo kwenye maji" ameeleza bw,Richard Komba manusura wa ajali hiyo.
Shughuli za kuaga miili 19 ya marehemu waliotokana na ajali hiyo itafanyika November 07,2022 katika Uwanja wa Kaitaba kuanzia majira ya saa 4 asubuhi ikifuatana na ibada.
Post a Comment