" TANGAZO KWA VIJANA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI TANZANIA – KURIPOTI CHUO CHA POLISI MOSHI

TANGAZO KWA VIJANA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI TANZANIA – KURIPOTI CHUO CHA POLISI MOSHI

 Polisi Tanzania

Polisi Tanzania

Majina Walioitwa Kujiunga na Jeshi la Polisi June 2025

Kamishna wa Jeshi la Polisi anawatangazia vijana walioteuliwa kujiunga na Jeshi la Polisi kuwa wanatakiwa kuripoti katika Chuo cha Polisi Moshi kuanzia tarehe 12/06/2025 hadi 14/06/2025 kwa ajili ya mafunzo.

MAELEKEZO KWA MAKUNDI MBALIMBALI YA VIJANA:

  1. Vijana waliofanyiwa usaili Dar es Salaam kwa ajili ya vikosi vilivyo chini ya Makao Makuu ya Polisi wanatakiwa kuripoti Dar es Salaam katika eneo la gwaride lililoko Kambi ya Polisi barabara ya Kilwa, nyuma ya Kituo cha Polisi Kilwa Road tarehe 12/06/2025 saa 6:00 mchana, kwa ajili ya kusafiri kuelekea Chuo cha Polisi Moshi.

  2. Vijana waliofanyiwa usaili katika mikoa ya Tanzania Bara wanatakiwa kuripoti kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa walikofanyiwa usaili tarehe 11/06/2025 saa 2:00 asubuhi ili kupewa taratibu za usafiri kwenda Chuo cha Polisi Moshi.

  3. Vijana waliofanyiwa usaili Zanzibar (Unguja na Pemba) wanatakiwa kuripoti Makao Makuu ya Polisi Zanzibar (Ziwani) tarehe 11/06/2025 saa 2:00 asubuhi kwa ajili ya maandalizi ya safari.


VIFAA VYA KUJILETA NAVYO:

  • Dera ya michezo ya rangi ya buluu yenye kola nyeupe

  • Fulana nyeupe isiyo na maandishi

  • Raba (viatu vya michezo), soksi nyeusi

  • Mifuko miwili ya michezo (duffel bags) ya buluu

  • Sanduku la bati la rangi ya buluu

  • Chandarua cheupe cha mduara (si cha pembe nne)

  • Mashuka manne ya buluu ya mwanga (light blue)

  • Pasi ya mkaa

  • Blanketi moja ya grey isiyo na maua (si duvet)

  • Kikombe cha plastiki (rangi cream light)

  • Sahani ya chuma

  • Vifaa vya usafi: Ufagio wenye mti, ndoo mbili ndogo, na sepetu

  • Kadi ya Bima ya Afya (NHIF) au pesa taslimu Tsh. 50,400/= kwa wasiokuwa na kadi

  • Vyeti vya taaluma halisi (Original), cheti cha kuzaliwa halisi, kadi ya NIDA au Kitambulisho cha Taifa

  • Nakala za NIDA za wazazi na ndugu wa karibu (baba, mama, babu, bibi, mjomba, shangazi, nk.)

  • Picha ndogo za pasipoti 6 (background ya buluu)

  • Nakala tano (5) za kila cheti kilichotajwa hapo juu

  • Fedha kwa matumizi binafsi (mahitaji ya maisha)


MAELEKEZO MUHIMU:

  • Simu za mkononi haziruhusiwi kabisa chuoni. Mtu yeyote atakayebainika kuwa na simu atachukuliwa kuwa amefanya kosa na atafukuzwa mara moja.

  • Taratibu za kupata namba za mawasiliano zitatolewa na chuo.

  • Mtu yeyote atakayefika Moshi baada ya tarehe 14/06/2025 hatapokelewa na atachukuliwa kuwa amejiondoa mwenyewe kwenye mafunzo.

Majina ya vijana waliopata nafasi ya kujiunga yanapatikana kwenye kiambatanisho cha tangazo hili.


Imetolewa na:

Kamishna wa Jeshi la Polisi Tanzania
Makao Makuu ya Polisi
S.L.P. 961, DODOMA

🔽 [BONYEZA HAPA KUPAKUA ORODHA YA MAJINA KATIKA PDF]


Post a Comment

Previous Post Next Post