Boaz Martine ambaye alikuwa mpiga picha wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga amefariki Dunia.
Na Mapuli Kitina Misalaba
Mtu mmoja amefariki dunia huku watu saba wakijeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyohusisha gari aina ya Toyota Harrier na Toyota Land Cruiser Hardtop mkoani Shinyanga.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Janeth Magomi amesema ajali hiyo ilitokea Mei 19, 2026 katika eneo la Kata ya Samuye, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa gari aina ya Toyota Harrier lenye namba T 210 EDB liligongana na Toyota Land Cruiser Hardtop yenye namba DFPA 8920 mali ya shirika la KOICA iliyokuwa ikisafirisha waandishi wa habari na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
SACP Magomi amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Toyota Harrier aliyekuwa akitokea Shinyanga kuelekea Tinde ambaye alijaribu kulipita gari lingine bila kuchukua tahadhari, hali iliyosababisha kugongana na Land Cruiser iliyokuwa ikiendeshwa na Laurence Peter (34).
Aliyefariki dunia ametambulika kwa jina la Boaz Martine ambaye alikuwa mpiga picha wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Miongoni mwa waliojeruhiwa ni askari Polisi Koplo Swahiba Msangi, Neema Madono (36), Rehema Edson (45), Shadia Omari (32), Laurence Peter (34), Johnson James pamoja na mwandishi wa habari wa ITV/Radio One Frank Mshana.
Majeruhi wote wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limetoa wito kwa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuendesha vyombo vya moto kwa tahadhari ili kuepusha ajali zinazoweza kusababisha madhara kwa wananchi.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment