Na Mapuli Kitina Misalaba
Mtu mmoja amefariki dunia huku watu saba wakijeruhiwa
katika ajali ya barabarani iliyohusisha gari aina ya Toyota Harrier na Toyota
Land Cruiser Hardtop mkoani Shinyanga.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi
la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Janeth
Magomi amesema ajali hiyo ilitokea Mei 19, 2026 katika eneo la Kata ya Samuye,
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa gari aina ya Toyota Harrier
lenye namba T 210 EDB liligongana na Toyota Land Cruiser Hardtop yenye namba
DFPA 8920 mali ya shirika la KOICA iliyokuwa ikisafirisha waandishi wa habari
na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
SACP Magomi amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa
dereva wa Toyota Harrier aliyekuwa akitokea Shinyanga kuelekea Tinde ambaye
alijaribu kulipita gari lingine bila kuchukua tahadhari, hali iliyosababisha
kugongana na Land Cruiser iliyokuwa ikiendeshwa na Laurence Peter (34).
Aliyefariki dunia ametambulika kwa jina la Boaz
Martine ambaye alikuwa mpiga picha wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Miongoni mwa waliojeruhiwa ni askari Polisi Koplo
Swahiba Msangi, Neema Madono (36), Rehema Edson (45), Shadia Omari (32),
Laurence Peter (34), Johnson James pamoja na mwandishi wa habari wa ITV/Radio
One Frank Mshana.
Majeruhi wote wanaendelea kupatiwa matibabu katika
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limetoa wito kwa
madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuendesha vyombo vya moto
kwa tahadhari ili kuepusha ajali zinazoweza kusababisha madhara kwa wananchi.
Boaz Martine ambaye alikuwa mpiga picha wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga amefariki Dunia.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment