" NIACHEKONA CUP 2026 KUENDELEA LEO MWABENDA, PICHA MBALIMBALI WAKATI WA UZINDUZI

NIACHEKONA CUP 2026 KUENDELEA LEO MWABENDA, PICHA MBALIMBALI WAKATI WA UZINDUZI

Na Mapuli Kitina Misalaba

Ligi ya NIACHEKONA CUP 2026 imeanza rasmi Mei 16, 2026 katika uwanja wa Mwabenda uliopo kata ya Solwa, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga huku ikihusisha jumla ya timu 22 kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya Mkoa wa Shinyanga.

Mashindano hayo yamezikutanisha timu kutoka Mkoa wa Mwanza, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Geita, Manispaa ya Shinyanga pamoja na timu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambayo ndiyo jimbo la Solwa.

Mchezo wa ufunguzi ulikuwa kati ya HOME BOYS dhidi ya MANHEIGANA ambapo timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 katika mchezo uliovutia mashabiki ambao waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa mashindano hayo.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa na Katibu wa Kamati ya Mashindano Sambayi Jilya, mchezo unaofuata utawakutanisha Wafukunyungu FC kutoka Manispaa ya Shinyanga dhidi ya Mwasenge kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga jimbo la Solwa.

Akizungumza katika uzinduzi wa mashindano hayo, mgeni rasmi ambaye ni Diwani wa kata ya Solwa Mhe. Dotto Samson amempongeza mwandaaji wa NIACHEKONA CUP 2026 kwa juhudi kubwa anazoendelea kuzifanya katika kuinua vipaji vya vijana kupitia michezo.

“Nikupongeze sana Niachekona, uthubutu ni jambo jema na hadi sasa dalili zilizopo umefaulu. Mwanzo huwa ni mgumu lakini kwa sasa jina lako limeendelea kuwa maarufu na liendelee kuwa maarufu kwa kuinua vipaji vya hawa vijana,” amesema Dotto Samson.

Aidha amesema anatamani mashindano hayo yawe chachu ya mafanikio kwa vijana wanaopenda mpira wa miguu huku akisisitiza kuwa michezo ni afya, ajira, burudani lakini pia ni biashara.

“Fanyeni kazi kwa malengo na muwe na nidhamu. Unapokuwa ndani ya uwanja hakikisha amani inakuwepo kwako na kwa mwenzako pia. Niwaombe mashabiki muendelee kuwa watulivu mnapokuwa uwanjani,” ameongeza.

Kwa upande wake mwandaaji wa mashindano hayo Bwana Paul Daud maarufu MC NIACHEKONA amesema kuwa huu ni msimu wa tatu wa mashindano hayo kufanyika katika uwanja wa Mwabenda kata ya Solwa.

“Hii ni awamu ya tatu kuandaa michuano hii hapa Mwabenda. Lengo kubwa ni kuwasaidia vijana kuachana na matukio yasiyo na maana na kuwaunganisha pamoja kupitia michezo huku wakielewa maana ya maisha na umuhimu wa amani,” amesema MC NIACHEKONA.

Ameongeza kuwa watu wengi humuita “Azam Mdogo” au “Jambo Mdogo” kutokana na namna anavyotumia nguvu na gharama kubwa kuhakikisha mashindano yanaendeshwa kwa ubora mkubwa ikiwemo maandalizi ya timu, usafiri pamoja na zawadi mbalimbali.

“Mimi kama mdau mkubwa wa michezo katika eneo hili ninaomba wadau mbalimbali ikiwemo Azam, Jambo FM na wengine waweze kunisapoti ili soka hili liendelee kukua na kusafiri salama,” amesema.

Pia amewashukuru wafadhili wake mbalimbali waliofanikisha kufanyika kwa mashindano hayo ya mwaka 2026 akiwemo Jambo FM kupitia kipindi cha Extra Time pamoja na Mabula Lushulwanhambi wa Mahembe ambaye amechangia maendeleo ya uwanja huo.

Mbali na michezo, MC NIACHEKONA ni Meneja wa Kishushu Hotel na pia ni mchimba madini katika mgodi wa Mwakitolyo. Kwa huduma za MC NIACHEKONA wasiliana naye kupitia namba 0757 267 738.

Kwa upande mwingine Polisi wa kata ya Solwa amewahakikishia wananchi usalama wa kutosha katika kipindi chote cha mashindano hayo.

RATIBA YA MECHI – NIACHEKONA CUP 2026

Mei 16, 2026
HOME BOYS Vs MANHEIGANA

Mei 17, 2026
WAFUKUNYUNGU FC Vs MWASENGE

Mei 18, 2026
DUARA FC Vs MWANDUTU

Mei 19, 2026
SHILIMA Vs SONGAMBELE MHANGU

Mei 20, 2026
NYUNDO FC Vs NZOZA

Mei 21, 2026
MAHEMBE Vs MAWEMIRU

Mei 22, 2026
NYANDOLWA Vs BAJAJ FC

Mei 23, 2026
SHILABELA Vs LYABUKANDE

Mei 24, 2026
KIMANDAGULI Vs KASHISHI

Mei 25, 2026
ISENENGEJA Vs MWAKITOLYO No.6

Mei 26, 2026
SANGU FC Vs BULIGE

Viongozi wakisalimiana na wachezaji kabla ya kuanza kwa mchezo wa NIACHEKONA CUP 2026.


SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 

Post a Comment

Previous Post Next Post