Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Salome Makamba amesema uzinduzi wa Mfumo wa Kidijitali wa Huduma za Mafuta wa PUMA - PRIS ni hatua muhimu katika kuimarisha uchumi wa kisasa unaotegemea teknolojia ndani ya sekta ya mafuta.
Amesema sekta ya nishati ni mhimili wa uchumi wa taifa, hivyo matumizi ya mifumo ya kidijitali yataongeza ufanisi wa huduma pamoja na kukuza matumizi ya teknolojia nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa PRIS (Puma Retail Information System), leo katika hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es salaam Mhe. Salome amesema mfumo huo ni teknolojia ya kisasa ya itakayosaidia kusimamia shughuli za vituo vya mafuta ikiwemo mauzo, malipo, usimamizi wa stoki za mafuta pamoja na taarifa za biashara kwa wakati halisi.
Ameeleza kuwa mfumo huo unalenga kuongeza ufanisi, uwazi na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wateja, sambamba na kuboresha usimamizi wa biashara za mafuta nchini.
Aidha, Mhe. Salome ameipongeza Puma Energy Tanzania kwa kuendelea kuwekeza nchini kupitia ubunifu wa kidijitali, upanuzi wa vituo vya mafuta na uwekezaji katika nishati safi ya CNG.
Amesema mfumo huo unaendana na malengo ya Tanzania ya kujenga uchumi wa kidijitali kupitia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 pamoja na Mkakati wa DESF 2024–2034.
Mfumo wa PRIS tayari umeonyesha mafanikio katika nchi za Malawi na Zimbabwe kabla ya kuanza kutumika Tanzania, huku Serikali ikieleza kuwa ubunifu huo utasaidia kuongeza ubora wa huduma na kukuza ujumuishi wa kiuchumi kwa wananchi.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254






Post a Comment