Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (BAWACHA) Mkoa wa Mara wamechangia kiasi cha Shilingi 1,000,000 kwa
ajili ya kusaidia ujenzi wa ukumbi wa vikao wa Ofisi ya CHADEMA Kanda ya
Serengeti.
Mchango huo umekabidhiwa na Mwenyekiti wa BAWACHA Mkoa
wa Mara, Veronica Sando, kwa niaba ya wanawake wote wa BAWACHA Mkoa wa Mara.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Bi. Veronica
amesema kuwa BAWACHA kupitia vikao vyao imeamua kuunga mkono juhudi za ujenzi
wa ukumbi huo ili kuhakikisha chama kinakuwa na kumbi zake wenyewe kwa ajili ya
shughuli mbalimbali pamoja na vikao vya chama.
Aidha, amesema kuwa mchango huo ni sehemu ya dhamira
ya wanawake wa BAWACHA katika kuimarisha miundombinu ya chama na kuendelea
kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya kisiasa na kijamii ndani ya chama
hicho.
Tukio la kukabidhi mchango huo limefanyika katika Jimbo la Kahama Mjini wakati wa maandalizi ya mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika jana, ambapo maelfu ya wananchi walihudhuria mkutano huo.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254







Post a Comment