Baraza la Watoto Ngazi ya Halmashauri, Kasulu Mji limeundwa rasmi baada ya uchaguzi wa viongozi wanne uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo kupambana na ukatili sambamba na kulinda haki za watoto.Katika uchaguzi huo, Elizabeth Bahati kutoka Shule ya Sekondari Kasulu amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo huku Boniphace Moshi kutoka Shule ya Sekondari Mwilamvya akichaguliwa kuwa Mwenyekiti Msaidizi.Viongozi wengine ni Augustino Emmanuel kutoka Shule ya Msingi Mdyanda aliyechaguliwa kuwa Katibu na Erasto Kamgisha Deusi kutoka Shule ya Sekondari Kigoma Grand akichaguliwa kuwa Mhasibu.Akizungumza baada ya uchaguzi huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu Mwl. Vumilia Julius Simbeye amewataka viongozi hao wapya kutumia nafasi zao kujifunza na kusimamia ipasavyo masuala ya haki za watoto bila woga."Serikali yetu chini ya Dkt. Samia inatambua uwepo wenu kwa hiyo niwaombe sana tunieni mabaraza haha kujitengenezea mazingira mazuri ya kujifunza lakini pia kama ambavyo mmechaguliwa na wenzenu basi simameni imara na msimamie haki zenu na za watoto wengine kwa sababj wote wanawategemea nyinyi"Kwa upande wake, Afisa Elimu Msingi kwa kushirikiana na Elimu Sekondari, Felician Ferdinand amewasisitiza watoto wote kutoa taarifa za ukatili na unyanyasaji sehemu husika ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.Katika hatua nyingine, Afisa Ustawi wa Jamii Salum Masaga amewataka viongozi wote kukusanya maoni kwa watoto ili kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali kulinda haki za watoto.Awali akiwasilisha mada ya mgawanyiko wa majukumu, Afisa Maendeleo ya Jamii Rebecca Mpango amewataka viongozi kutekeleza majukumu yao kwa uwajibikaji na weledi.





SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254











Post a Comment