Na
Mapuli Misalaba, Shinyanga
Askofu wa makanisa ya Africa Inland Church
Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zakayo Bugota amesema
changamoto za maisha hutengeneza aibu kwa kila mtu hivyo amewataka wakristo
kufanya kazi kwa bidii ili kuimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja.
Ameyasema hayo wakati akihubiri kwenye ibada ya
Jumapili katika kanisa la AICT Kambarage mjini Shinyanga ambapo amewakumbusha
wakristo kufanya kazi, kuondoa uvivu pamoja na kumtanguliza Mungu katika maisha
ya kila siku.
Askofu Bugota ametumia fursa hiyo kuwasisitiza
wakristo wote kujenga utaratibu wa kumshukuru Mungu kwa kila jambo na kufanya maombi ya kuombea
kizazi cha ulimwengu huu ili kukua katika maisha yanayompendeza Mungu.
“Mungu ametubariki kwa neema yake tunapokuwa
kwenye maoni ni muhimu sana kukiombea
kizazi ili uzao uwe na baraka jumuishi, mimi ninaamini maombi tunayofanya Mungu
ataleta matokeo na majibu yake yatakuwa
na baraka ambazo zitawagusa wengine”.
“Unapobarikiwa
maana yake unatakiwa uwaombee na wengine wapate hizo baraka majibu ya Bwana
lazima yatengeneze furaha na shangwe ambazo zitatengeneza baraka za jumla
katika maisha”.amesema Askofu Bugota
Askofu Bugota amewakumbusha wakristo wote na jamii
kwa ujumla kuacha dhabi na kumrudia
Mungu hasa nyakati hizi kuelekea kuzaliwa kwa Yesu kristo ili aweze kujibu mahitaji ya kila mtu.
Askofu wa makanisa ya Africa Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zakayo Bugota akihubiri kwenye ibada ya Jumapili leo Desemba 18,2022.
Waumini wakisikiliza mahubiri katika ibada ya Jumapili
Post a Comment