Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Msimamizi msaidizi wa uchaguzi
mdogo kata ya Mwamalili,Jimbo la uchaguzi Shinyanga Mjini,Bwana Aden Isack Mwakatage amemtangaza James
Mdimi wa chama cha Mapinduzi kuwa ndiye
Mshindi wa nafasi ya udiwani katika kata hiyo.
Mdimi wa CCM ametangazwa kuwa
diwani wa kata ya Mwamalili,baada ya kupata kura 3,126 dhidi ya mpinzani wake Yunja Machiya wa chama Cha ACT
wazalendo ambaye amepata kura 76.
Idadi ya wapiga kura walikuwa 3934 waliopiga kura ni
3214 kura zilizoharibika ni 12 ambapo kura halali zilikuwa 3202.
Uchaguzi huo umefanyika jana jumamosi ili kuziba pengo lililoachwa wazi na aliyekuwa diwani wa kata hiyo Paulo Machela ambaye alifariki dunia Januari 1,2021.
Post a Comment