" JWTZ KANDA YA SHINYANGA WAFANYA SHUGHULI ZA KIJAMII KUADHIMISHA MIAKA 61 YA UHURU

JWTZ KANDA YA SHINYANGA WAFANYA SHUGHULI ZA KIJAMII KUADHIMISHA MIAKA 61 YA UHURU

Jeshi la Wananchi wa Tanzania Mkoa wa Shinyanga leo limeadhimisha Miaka 61 ya Uhuru wa Tanganyika kwa kushiriki katika shughuli mbali mbali za kijamii ikiwemo upandaji wa miti na usafi wa mazingira katika maeneo mbali mbali ya Manispaa ya Shinyanga

Mkuu wa vikosi vya Jwtz kanda ya Shinyanga kanali Machuza Alex Sunzu amesema askari wa Jeshi hilo wameadhimisha siku hii kwa kupanda miti 400 katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Shinyanga na kwamba maadhimisho hayo yalianza tangu Disemba 02,kwa kushiri katika shughuli za usafi wa mazingira katika maeneo mbali mbali ikiwemo kwenye taasisi za serikali kwa kushirikiana na Wananchi

Akizungumza baada ya kupanda miti hiyo afisa wa jeshi la wananchiwa Tanzania Jwtz, meja Ndyamkama kente amewaomba wakazi wa Shinyanga kutunza miti iliyopandwa ili kuhifadhi mazingira

Kwa upande wake Afisa maliasili na mazingira wa Manispaa ya Shinyanga Bwana Ezra Manjerenga, ambaye ameshirikiana na askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kanda ya Shinyanga amesema lengo  la kupanda miti katika siku ya kumbukumbu ya Uhuru ni kuhakikisha uhuru unadumishwa katika mazingira safi na salama

Leo Disemba 09,2022 watanzania wameadhimisha kumbukumbu ya Miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara,ambapo Mkoa wa Shinyanga umeadhimisha kwa namna mbalimbali ikiwemo kufanya midahalo, makongamano na kushiriki katika shughuli za kijamii ikiwemo kupanda miti na usafi wa mazingira.

Mkuu wa vikosi vya Jwtz kanda ya Shinyanga kanali Machuza Alex Sunzu. afisa wa jeshi la wananchiwa Tanzania Jwtz, meja Ndyamkama kente.

Afisa maliasili na mazingira wa Manispaa ya Shinyanga Bwana Ezra Manjerenga

 













Post a Comment

Previous Post Next Post