Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Mkuu wa Magereza Mkoa wa
Shinyanga kamishna msaidizi wa Magereza Josephine Semwenda na Mkuu wa
Gereza la Wilaya ya Shinyanga William
Makwaya kwa kushirikiana na maaskari wao wameadhimisha Miaka 61 ya uhuru wa
Tanganyika kwa kufanya usafi wa Mazingira katika maeneo mbalimbali ya Manispaa
ya Shinyanga.
Shughuli hiyo ya usafi wa
Mazingira imefanyika leo Disemba 9, 2022 majira ya Asubuhi ikiwa ni kilele cha
siku ya Uhuru wa Tanganyika kutimiza Miaka 61 hapa Nchini.
Akizungumza baada ya kushirika
shughuli hiyo, Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Shinyanga William Makwaya amesema
wamehamasika kuungana na watanzania wengine kuitumia vyema siku hii kwa
kushirika shughuli mbalimbali ikiwemo kufanya usafi wa Mazingira.
Aidha Mkuu huyo amesema
katika eneo lao tayari wameshapanda miti zaidi ya Elfu kumi kwa lengo la kupendezesha mazingira ya Mji wa
Shinyanga.
“Tumeadhimisha
siku hii kwa kufanya usafi katika eneo letu tumefanya usafi kambini, tumeufanya
katika uwanja wetu wa mazoezi lakini pia tumefanya usafi katika msikiti uliopo
karibu na magereza kwa ujumla tumesherehekea vizuri na tumehamasika kujua
kwamba tuko pamoja na serikali yetu katika kuhakikisha kwamba kila kitu
kinakwenda kulingana na taratibu, sheria na kanuni”.amesema
Makwaya
“Mkoa
wetu wa Shinyanga unahitaji sana kupanda miti ili turudishe uoto wa asili na
sisi kama magereza tumehamasika na tumepanda miti zaidi ya Elfu kumi kuzunguka
eneo letu na tunaitunza tunahakikisha kwamba baada ya miaka kadhaa itakuwa
imefikia hatua ya kutoa kivuli na matunda kwa lengo la kuibadilisha kuwa Shinyanga
ya kijani”.amesema Mkuu wa Gereza Wilaya ya
Shinyanga Makwaya
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Magereza Josephine Semwenda na Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Shinyanga William Makwaya wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumaliza zoezi la kufanya usafi wa Mazingira.TAZAMA PICHA ZOTE HAPA CHINI
Post a Comment